Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kati Dk. Syprian Yohana Hilinti (katikati) akiwa mbele ya maaskofu wakati wa ibada ya kuwekwa Wakfu iliyofanyika Kanisa la Emmanuel Msalaba Mrefu Mjini Singida leo Oktoba 30,2022.
Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kati Dk. Syprian Yohana Hilinti akivikwa pete ya kiaskofu katika ibada hiyo.
Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kati Dk. Syprian Yohana Hilinti akivikwa kofia ya kiaskofu katika ibada hiyo.
Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kati Dk. Syprian Yohana Hilinti akibarikiwa na maaskofu katika ibada hiyo.

Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kati Dk. Syprian Yohana Hilinti akikabidhiwa fimbo ya kiaskofu.
Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kati Dk. Syprian Yohana Hilinti akimpongeza Msaidizi wake Mteule Mchungaji Dk. Zephania Nkesela wakati wa ibada hiyo, iliyoongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa hilo nchini Dk.Fredrick Shoo..
Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba akisoma hutuba kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan katika ibada hiyo.
Ibada ikiendelea.
Ibada ikiendelea.
Ibada ikiendelea.
Ibada ikiendelea.
Kwaya ya Matarumbeta kutoka Ujerumani ikitoa burudani.
Kwaya ikitoa burudani.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba (wa tatu kutoka kulia) akiwa na viongozi mbalimbali katika ibada hiyo.
Kwaya ikitoa burudani.
Maaskofu wakiwa tayari kwa kumuweka Wakfu Askofu Mteule, Dk. Sprian Hilinti.
Wachungaji wakiwa kwenye ibada hiyo.
Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kati Dk. Syprian Yohana Hilinti akiwekwa Wakfu.
Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kati Dk. Syprian Yohana Hilinti (wa pili kulia)akipongezwa baada ya kusimikwa.



Katibu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Mhandisi Robert Kitundu akizungumza kwenye ibada hiyo.,
Waumini wa kanisa hilo wakimshukuru Mungu kwa tendo hilo.
Maaskofu wakitoa baraka kwa Askofu Mteule Dk.Sprian Hilinti.
Mke wa Askofu Mteule akimvika shada la maua mumu wake.


Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kati Dk. Syprian Yohana Hilinti (katikati) akisaini hatiya utumishi.


Kwaya ikitoa burudani.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba (wa tatu kutoka kushoto) ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) baada ya ibada hiyo.
Picha ya pamoja na wageni waalikwa kutoka Ujerumani.
Picha ya pamoja ya ndugu, jamaa na marafiki wa viongozi hao wateule.
Picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.
Picha ya pamoja na maaskofu.
Picha ya pamoja ndugu, jamaa na marafiki wa viongozi hao wateule.

Na Dotto Mwaibale, Singida.

SERIKALI imesema itaendelea kushirikiana na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na kuhakikisha wanaendelea kutoa huduma bora za maendeleo kwa wananchi hususani katika miradi ya elimu na afya.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba ameyasema hayo kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan katika ibada ya kumweka Wakfu na kumsimika Askofu Mteule Dk. Syprian Hilinti kuwa Askofu wa Kanisa la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kati pamoja na kumwingiza kazini Msaidizi wa Askofu Mteule Mchungaji Dk. Zephania Nkesela ibada iliyoongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa hilo nchini Dk.Fredrick Shoo.

“Serikali inatambua na kuthamini mchango wa Kanisa la KKKT katika huduma za kiroho, kuhubiri injili ya amani, umoja, haki na kweli” alisema Serukamba.

Alisema kanisa hilo pamoja na kutoa huduma za kiroho linatoa pia huduma mbalimbali za kijamii zikiwemo huduma za elimu na afya kwa kushirikiana na serikali akitolea mfano huduma za Hospitali ya Ihambi iliyopo wilayani Mkalama ambapo Serikali inawalipa mshahara watumisi 31 ili kuwezesha malengo ya kanisa kwa kutoa huduma kwa wananchi bila ya kujali imani zao.

Akizungumza baada ya kusimikwa rasmi kuwa Askofu, Dk. Sprian Hilinti aliipongeza Serikali kwa kuendelea kuleta maendeleo kwa jamii kama ujenzi wa vyuo vya ufundi stadi vya VETA na kuwa jambo ilo linavumbua, kulea na kutia moyo vipawa na kanisa litaendelea kuwatia moyo na kuwaambia watu kuwa mambo yote yanawezekana.

Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT, Dk. Fredrick Shoo akizungumza wakati wa ibada ya kuwasimika viongozi hao wateule aliwataka kuzingatia taratibu za kanisa katika uongozi wao na kujishusha wakati wote badala ya kujikweza.

Aidha Askofu Shoo alitoa angalizo kwa wanasiasa kuacha kujaribiwa kwa kuchukulia dini kama taasisi zisizo za kiserikali kwa maana ya kuilinganisha dini na NGO’S.

“Nawaombeni msijaribiwe katika jambo hili iwe Kanisa au Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) msithubutu kuzifanya kama NGO’S” alisisitiza Dk.Shoo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: