Benki ya CRDB imetangaza kuanzisha programu ya uwezeshaji kwa vijana na wanawake wajasiriamali ikiwa na lengo la kukuza ujumuishi wa kiuchumi nchini.

Taarifa hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kongamano la sita la TEHAMA (TAIC) linalofanyika visiwani Zanzibar kwa muda wa siku tatu kuanzia leo 26 hadi 28 Oktoba 2022.

Kongamano hilo limezinduliwa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, na taasisi kutoka ndani na nje ya nchi.

Nsekela alibainisha kuwa kwa kushirikiana na Tume ya TEHAMA, katika kongamano hilo Benki ya CRDB inakwenda kuzindua programu wezeshi kwa wajasiriamali vijana na wanawake wenye biashara na mawazo bunifu katika sekta mbalimbali ikiwamo sekta TEHAMA iliyopewa jina la “IMBEJU”.

Benki ya CRDB ni mdhamini mkuu wa Kongamano la TAIC 2022 ambalo limepewa kauli mbiu ya“Mabadiliko ya Kidijitali kwenye Uchumi wa Buluu kwa Maendeleo ya Jamii na Kiuchumi”.
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi akimkabidhi cheti cha udhamini mkuu wa Mkutano wa Mwaka wa Sekta ya TEHEMA, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela katika hafla ya ufunguzi wa mkutano huu unaofanyika katika hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar kuanzia leo Oktoba 26 hadi 28, 2022. Kulia ni Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano, na Uchukuzi Zanzibar, Dkt. Khalid Salum.
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi akizungumza wakati akitoa hotuba yake katika hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Sekta ya TEHEMA nchini, ulioanza leo kwenye hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar. Mkutano huo utafanyika kwa siku tatu kuanzia leo Oktoba 26 hadi 28, 2022.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Sekta ya TEHEMA nchini, ulioanza leo kwenye hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar. Mkutano huo utafanyika kwa siku tatu kuanzia leo Oktoba 26 hadi 28, 2022.


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Sekta ya TEHEMA nchini, ulioanza leo kwenye hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar. Mkutano huo utafanyika kwa siku tatu kuanzia leo Oktoba 26 hadi 28, 2022.





Sehemu ya washiriki wa Mkutano wa Mwaka wa Sekta ya TEHEMA nchini, ulioanza leo kwenye hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar. Mkutano huo utafanyika kwa siku tatu kuanzia leo Oktoba 26 hadi 28, 2022.



Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi akipata maelezo kuhusu huduma za kidijitali zinazotolewa na Benki ya CRDB kutoka kwa Meneja wa Tawi la Benki hiyo Michenzani Zanzibar, Ahmad Aboubakar (kushoto) wakati alipotembelea banda la Benki ya CRDB katika uzinduzi wa Mkutano wa Mwaka wa Wadau wa Sekta ya TEHEMA unaofanyika katika hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar kuanzia leo Oktoba 26 hadi 28, 2022. Wengine pichani ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye (wapili kulia), Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, Dkt. Khalid Salum (watatu kulia), na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: