Umoja wa Machinga mkoani Iringa umesema kuwa ziara ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mkoani Iringa ni fursa ya kipekee kwa kundi hilo kuwasilisha shukrani zao kwa serikali kufuatia bajeti ya iliyosomwa bungeni ya kiasi cha zaidi ya bilioni 40 zitakazoelekezwa katika kusaidia mikopo kwa kundi hilo.
Katibu wa Umoja wa Machinga mkoani Iringa Joseph Kirienyi Mwanakijiji akizungumza na vyombo vya habari amesema kupitia maelekezo ya Mhe. Rais kundi, hilo la Machinga limefufua matumaini makubwa ya kukuza mitaji yao na kujikwamua kiuchumi.
Mwanakijiji amesema kuwa Wamachinga wanayofuraha kubwa kwa ujio wa Rais Mkoani Iringa kwani wanaona mwanga wa maendeleo zaidi na kutambulika rasmi kwa kundi hilo katika fursa mbalimbali zitakazochochea maendeleo
Kiongozi huyo wa Machinga Mkoani Iringa amemtaja Rais Samia Kuwa Mama mwenye kujali maslahi ya wanyonge kupitia matamko mbalimbali anayoyatoa ikiwemo yale ya kuwataka wakuu wa mikoa,wilaya na wakurugenzi kutumia hekima kuwapanga wamachinga katika maeneo rafiki ya kufanyia biashara hatua iliyoendeleza utulivu katika maeneo mbalimbali hususani Mkoani Humo.
Katibu wa Machinga Joseph Kirienyi ameongeza kuwa kulingana na namna Rais Samia anavyowakumbuka wamachinga, Kundi hilo kwa pamoja limekubaliana kundaa mabango ya kumpokea Rais yenye ujumbe wa kumshukuru, kumpongeza na kumuombea katika utekelezaji wa majukumu yake katyika kulingenga taifa
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja huo Yahaya Mpelembwa amesema Ujio wa Rais Samia Suluhu Hassan mkoani Iringa utachochea kasi ya Utatuzi wa Changamoto mbalimbali kwa kundi hilo ikiwemo kukamilishwa kwa ujenzi wa vibanda vya biashara katika eneo la mlandege kabla ya maazi ya wafanyabiashara hao kuhamishwa kutoka maeneo wanayofanyia biashara kwa sasa.
Nao baadhi ya wamachinga Akiwemo Shamira Mohamedi na Huruma Chusi wamemuomba Rais Samia katika ziara yake hiyo atembelee Soko la Mlandege ili kujionea hali halisi ya maendeo yanayoandaliwa kwa ajili ya Wafanyabiahara hao wadogo (Machinga),
Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuanza ziara yake siku tatu mkoani Iringa mnamo Agosti 11 hadi 13 Mwaka huu ambapo akiwa mkoani humo atakagua miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi katika maeneo mbalimbali.
Toa Maoni Yako:
0 comments: