Kutoka kushoto ni Rais wa CAF Patrice Motsepe akiwa na Rais wa FIFA Gianni Infantino wakati wa uzinduzi wa Africa Super League.

Infantino aliulizwa kuhusiana na Afrika kuwahi kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia mara moja tu (2010 Afrika Kusini) anatusaidiaje kuona Afrika inapata nafasi ya kuwa mwenyeji tena.
Rais wa Shirikisho la soka Duniani (FIFA) Gianni Infantino wakati wa mkutano wa 44 wa CAF ambapo Mgeni Rasmi akiwa Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa aliongea na waandishi wa habari na kuulizwa maswali kadhaa.
Rais wa FIFA Gianni Infantino akiwa katika mkutano wa 44 wa CAF

“Tupo hapa pia kwa ajili ya hilo tunataka Afrika iwe mwenyeji wa michuano mingi mikubwa ya kidunia kama alivyosema Motsepe”Kutoka kushoto Rais wa FIFA Gianni Infantino akiteta jambo na Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa

“Hata AFCON sasa ni michuano mikubwa ya kidunia na ina wachezaji wakubwa wanaofanya vizuri katika vilabu bora duniani ni wachezaji wanaotokea Afrika”Wajumbe wa Mkutano wakisikiliza hotuba ya Rais wa CAF Patrice Motsepe

Hata hivyo kwa upande wa Rais wa Shirikisho la soka Afrika (CAF) Patrice Motsepe amesema moja kati ya vitu watajadili ni pamoja na ombi la Tanzania la kutaka kuwa mwenyeji wa fainali za mataifa ya AFCON kwa kushirikiana na jirani yake Uganda.Kutoka kushoto ni Rais wa CAF Patrice Motsepe akmkabidhi bendera ya CAF Rais wa Shirikisho la soka Tanzania TFF Wallace Karia

“Kuna vitu muhimu tunaenda kujadili, kama nilivyosema tunaenda kujadili kuhusiana na Maendeleo ya soka lakini moja kati ya jambo kubwa ni kwamba Tanzania inataka kuwa mwenyeji wa AFCON wakishirikiana na Uganda, Kama unakuwa mwenyeji wa AFCON hii ni michuano mikubwa ya kidunia”>>> Motsepe
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: