Mgombea wa nafasi ya Urais nchini Kenya, William Ruto ambaye ni Makamu wa Rais nchini humo, kutoka Chama cha United Democratic Party (UDP) akipiga Kura katika Kituo cha Shule ya Msingi Kosachei. (Picha na Baz Ratner | Reuters).
Mgombea wa nafasi ya Urais nchini Kenya, Raila Odinga ambaye alikuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo, akipiga Kura katika Kituo cha Shule ya Msingi Kibera mjini Nairobi. (Picha na Thomas Mukoya | Reuters).
Rais anayemaliza muda wake, Uhuru Kenyatta mapema leo akielekea kupiga Kura nyumbani kwao, Gatundu. (Picha na Eramo Egbejule | Al Jazeera).
Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
KENYA imeingia kwenye Uchaguzi Mkuu, Agosti 9, 2022 kumchagua Rais mpya wa nchi hiyo ambaye atachukua nafasi ya Rais anayemaliza muda wake, Uhuru Kenyatta ambaye alihudumu kwenye nafasi hiyo ya Urais tangu Aprili 9, 2013.
Katika Uchaguzi huo, Wagombea wanaopewa nafasi kubwa ya kumrithi, Uhuru Kenyatta ni William Ruto ambaye ni Makamu wa Rais wa sasa wa nchi hiyo tangu mwaka 2013, Ruto ni Kiongozi wa Chama cha Siasa nchini humo cha United Democratic Party (UDP), Kenya Kwanza Alliance.
Pia nafasi hiyo inawaniwa na Aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo (2008-2013), Raila Ondinga ambaye ni Kiongozi wa Chama pinzani cha Orange Democratic Movement (ODM) kilicho chini ya Azimio la Umoja, One Kenya Alliance.
Katika Kampeni zao kuelekea Uchaguzi huo, kila Mgombea ametoa vipaumbele vyake ili kuikomboa na kuleta maendeleo nchini Kenya, William Ruto ametoa kipaumbele cha kuimarisha Uchumi ili kuboresha maisha ya Wananchi wa nchi hiyo, wakati Raila Odinga akiwa na kipaumbele cha kuleta Umoja wa Kitaifa na Ustawi wa watu wake.
Wakiwa na matarajio makubwa ya kuingia kwenye Ofisi ya Rais (White House), Wagombea hao wanaongozana na Wagombea wenza kuwania nafasi hiyo, William Ruto anaambatana na Mgombea Mwenza, Mwanasheria, Martha Karua na Mgombea, Raila Odinga anaambatana na Mgombea mwenza, Rigathi Gachugua.
Hata hivyo, wapo Wagombea wengine ambao ni Kiongozi wa Roots Party of Kenya, Prof. George Wajackoyah na David Waihiga Mwaure ambaye ni Kiongozi wa Agano Party.
Wagombea hao mapema leo wamepiga Kura sehemu mbalimbali nchini humo, kupitia Vituo mbalimbali vilivyotengwa kwa ajili ya Uchaguzi huo, Mgombea, William Ruto mapema leo, amepiga Kura kwenye Kituo cha Shule ya Msingi Kosachei.
Mgombea, Raila Ondinga amepiga Kura kwenye Kituo cha Shule ya Msingi Kibera mjini Nairobi, huku Mgombea mwengine Prof. George Wajackoyah akipiga Kura yake Kituo cha Matungu katika Kaunti ya Kakamega sanjari na Mgombea David Waihiga Mwaure aliyepiga Kura kwenye Kituo cha Upper Hill, mjini Nairobi.
Kwenye Uchaguzi huo, Wakenya wanatarajiwa kuchagua Wabunge, Maseneta, Magavana wa Kaunti na Wajumbe 47 wa Kaunti za Kenya.
Zaidi ya Wakenya Milioni 22 (22,120,458) wanatarajiwa kupiga Kura kwenye Uchaguzi huo, Uchaguzi wa nchi hiyo unasimamiwa na ‘Independent Electoral and Boundaries Commission’ - Tume ya Uchaguzi na Mipaka ya nchi hiyo (IEBC).
Toa Maoni Yako:
0 comments: