Ofisa wa Mashirikiano wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), Nima Sitta akizungumza mkakati wa shirika hilo katika kwenda kusaidia wakulima kwenye maonesho ya kilimo Kitaifa yanayofanyika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV Mbeya
SHIRIKA la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limetenga dola 15000 milioni kwa ajili ya mradi wa miaka mitano unaotambulika kwa jina la Master card Foundation ambapo unalenga kuwasaidia wakulima wa mbogamboga na matunda ili waondokane na kilimo cha mazoea.
Haya yameelezwa na Ofisa Mashirikiano wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Nima Sitta kwenye maonesho ya wakulima kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Amesema kuwa WFP imejipanga kuwasaidia wakulima katika nyanja tofauti kupitia mradi wao waliouzindua hivi karibuni wa Master card Foundation utakaodunu kwa muda wa miaka mitano unaoshia 2030.
Sitta amesema katika kusaidia Serikali kufikia malengo 10/30 Kama shirika kupitia miradi wanayoianzisha wana mpango wa kumuwezesha mkulima atambue kuwa kilimo ni biashara ambapo wanawasaidia kuwapatia elimu, kuwakutanisha na taasisi za fedha ili wakulima wakopesheke, kuwasimamia katika uzalishaji,kuwasaidia katika miundombinu ya umwagiliaji na kuwatafutia masoko ya uhakika pale wanapovuna mazao.
Amesema shirika limepanga kuwafikia wakulima zaidi ya 100,000 katika kwa kipindi cha miaka miwili ijayo kwa kuhakikisha wanawasaidia wakulima ili kuondokana na kilimo cha mazoea ambapo baadhi ya mikoa walianza kuwasogezea fursa hiyo kuwa Dodoma,Singida,Simiyu,Tabora na Mara kwa kilimo cha mtama ambapo Soko lake liko Sudan Kusini
Akizungumzia kuhusiana na walivyojipanga kuwafikia vijana kwenye mradi wa Building Better Tommorow uliozinduliwa na Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa amesema Kama wadau wakuu wa chakula wamekuwa wakizungumza na wadau na makundi mbalimbali ya vijana iliwaweze kutambua kuwa kilimo ni biashara na kuwahamasisha waweze kujiunga kwenye makundi ili waweze kukopeshwa mitaji.
Aidha amesema mbali na kutoa msukumo huo kwa Wakulima wa mbogamboga pia watoa msukumo kwa wakulima wa ngano na mpunga.
Toa Maoni Yako:
0 comments: