Mgeni Rasmi, Naibu Katibu Mkuu (TAMISEMI) Bw. Ramadhani Kailima (wa tatu toka kushoto), Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Seka Urio (wa pili kulia), Afisa Mkuu wa Masoko Multichoice Tanzania, Shumbana Walwa, (wa pili toka kushoto) na Tracy kutoka Kids Finance with Tracy (wa kwanza kushoto) wakipata maelezo kwa mtoto anayefanya biashara mara baada ya kumtebelea katika maonyesho hayo.
Mgeni Rasmi, Naibu Katibu Mkuu (TAMISEMI) Bw. Ramadhani Kailima (wa pili toka kushoto) akiwa na Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Seka Urio (wa pili kulia), wakipata maelezo kwa mtoto anayefanya biashara mara baada ya kumtebelea katika maonyesho hayo.
Mabinti ambao waliudhuria maonyesho ya wajasiriamali hapo jana jijini Dar esSalaam.
Binti wajasiriamali akiwa katika nyuso ya furaha.
Tracy Makoi wa Kids Finance with Tracy akimpatia cheti mtoto John nelly aliyekuwa mshirika wa maonyesho hayo ya Business fair hapo jana jijini Dar es Salaam.
Watoto walioshiriki maonyesho ya wajasiriamali vijana wakiwa katika picha ya pamoja



Wajasiriamali vijana wamefanya maonyesho ya biashara kwa mara ya tatu ambayo yamehusisha biashara mbalimbali zilizoanzishwa na vijana wadogo.

Maonyesho hayo ya biashara yaliyofanyika mapema jana katika Mgahawa wa Mtana, uliopo Oysterbay, Dar es Salaam yaliandaliwa na Kids Finance, Jengahub na Natokajekidijitali na kushirikisha vijana wadogo wenye umri wa kati ya miaka 8 hadi 17 na Tracy kutoka Kids Finance.

Vijana wengi wamekuwa na shauku ya kupata mafanikio kama ilivyo kwa wazazi wao ili kuhakikisha wanatimiza ndoto zao na kuziletea mabadiliko kwa jamii. Wajasiriamali hao wadogo, hutufundisha jinsi ya kuchimba kwa kina ili kufichua malengo yetu na kufikiria jinsi tunavyoweza kutumia malengo hayo kuanzisha biashara. Hii ni fursa pekee kwa vijana wajasiriamali kwa ajili ya kuwaunga mkono katika katika biashara zao.

Tunapowaunga mkono wajasiriamali hawa wadogo ambao tunawapa fursa ya kutengeneza ajira hapo badaaye katika sekta binafsi.

Pia tunawahimiza vijana wadogo wengine kutokata tamaa ili kuhakikisha wanajiajiri kwa hapo baadaye. Wazazi wanahimizwa kuleta vijana wao kuja kuwaona wenzao wakionyesha biashara zao katika maonyesho haya, pia wanaweza kujifunza zaidi kuhusu biashara nyingine, kutiwa moyo na kujifunza ujuzi mpya.

"Natumaini kwamba watatiwa moyo na kupewa ushirikiano, bado hujachelewa kufanya kazi katika biashara ya ndoto zako,’ alisema

Mkurugenzi Mtendaji wa Jengahub, Nancy Sumari anasema: “Tumefurahishwa na maonyesho haya ya biashara na tunawakaribisha vijana na watoto wote kuja kutembelea mabanda mbalimbali. Kuna mengi ya kujifunza, na huu ni mwanzo kwao. Kwa hivyo, tunakaribisha kila mtu kuhudhuria maonyesho ya biashara.

Kama Natokajekidigitali tunaamini kwamba kwa sasa kuna umuhimu wa vijana wagogo kupata ujuzi kidijitali ili kukuza fursa mpya mitandaoni na kuongeza uwezo wa kufikiri. Pia watafundishwa michezo mbalimbali inayoongeza uwezo wa mtoto kufikiri, kuweka mikakati na kuchambua mambo mbalimbali ikiwemo michezo ya kisasa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: