Simba Queens SC imefuzu kwenda Morocco kucheza fainali za CAF Champions League kwa soka la wanawake baada ya kuifunga She Corporate ya Uganda kwa goli 1-0 katika mchezo wa fainali wa Michuano ya mchujo ya CAF ukanda wa CECAFA, (CECAFA Zone Qualifiers) uliopigwa katika uwanja wa Azam Complex Chamazi usiku wa kuamkia leo Agosti 28, 2022.
Bao la Simba Queens SC lililofungwa na Vivian Corazone kwa mkwaju wa penati dakika ya 49, baada ya Asha Djafari kufanyiwa madhambi kwenye eneo la hatari.
Michuano hiyo ya CAF Champions League Unatakiwa kuanza mwezi ujao, na huwa inachezwa katika taifa moja ikijumuisha jumla ya timu 8, sita mabingwa kutoka zone sita za soka, nafasi moja ya Bingwa mtetezi na nyingine Bingwa wa nchi mwenyeji.
Toa Maoni Yako:
0 comments: