Afisa Mkuu Mauzo na Masoko wa Shirika la Nyumba la Taifa, Bw. Emmanuel J. Lyimo akizungumza na mwananchi waliotembelea banda la maonesho la Shirika la Nyumba la Taifa mapema jana katika viwanja vya John Mwakangale mkoani Mbeya.

Mwandishi Wetu, Mbeya

MRADI mpya wa Nyumba 400 zitakazojegwa katika eneo la Kawe jijini Dar es Salaam umekuwa kivutio kwa wananchi mbalimbali wanaofika katika Maonyesho ya Wakulima Nanenane kwenye banda la Shirika la Nyumba la Taifa lililopo kwenye viwanja vya John Mwakangale katika eneo la Kijiji cha Serikali jirani kabisa na eneo la Magereza.

Mradi huo umegeuka darasa la wananchi wengi kupata taarifa za kuanza kwake na namna utakavyotekelezwa na hata unafuu wa gharama zake.

Akizungumza katika banda hilo, Mhandisi Benedict Ndunguru amesema amevutiwa na bei ya nyumba aina ya studio pamoja na muundo wa nyumba za mradi wa Kawe.

Amesema pia kuwa vipaumbele vitakavyozingatiwa katika ujenzi wa nyumba hizo za ghorofa hususani ukubwa wa vyumba na gharama zake ni jambo litakalosaidia watanzania wengi kuweza kumiliki nyumba katika mradi huo.

Nao Nicholaus Malakasuka na Alex Siuzuguye wamesema kuwa wamevutiwa na mradi mpya wa Uptown Kawe kwa kuwa na machaguo mengi kwa nyumba ya vyumba viwili na kimoja ambapo mnunuzi anaweza kununua aidha nyumba ya vyumba viwili au akanunua nyumba ya vyumba vitatu na au chumba kimoja.

Wamesema ubunifu huo wa machaguo uliofanywa na Shirika unawapa Watanzania fursa nyingi zaidi ya kujipatia machaguo ya nyumba kulingana na vipato vyao tofauti tofauti.

Ujenzi wa nyumba 400 katika eneo la Kawe kwa ajili ya wananchi wa kipato cha kati cha chini utaanza baadaye mwezi huu. Mpango wa ujenzi huu ni sehemu ya mpango wa ujenzi wa nyumba 5,000 zitakazojengwa nchi nzima.

Akizungumza katika maonyesho hayo Afisa Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Shirika la Nyumba la Taifa, Emmanuel J. Lyimo amesema kuwa mradi huo wa aina yake ni sehemu ya Mpango wa Shirika kuweza kuwafikia Watanzania wengi zaidi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: