Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Shinyanga Madini Marathon, Roland Mwalyambi (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema Jezi ya uhamasishaji wa Shinyanga Madini Marathon 2022.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mbio za Shinyanga Madini Marathon 2022 zilizoandaliwa na Klabu ya Mazoezi maarufu Police Jamii Fitness Center Shinyanga (PJFCS) inayolelewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga zinatarajiwa kufanyika Agosti 7,2022 Mjini Shinyanga.

Akizungumza leo Ijumaa Aprili 8,2022 wakati Kamati ya Maandalizi ya Shinyanga Madini Marathon ilimpotembelea Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema kwa ajili ya kujitambulisha na Kukabidhi Jezi ya uhamasishaji pamoja andiko la mbio, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Roland Mwalyambi amesema maandalizi yanaendelea vizuri.

“Tumefika hapa katika Ofisi yako Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mama yetu Sophia Mjema kwa ajili ya kujitambulisha kwako na kuomba ridhaa ya kufanya Mbio za Marathon na kukabidhi Jezi ya uhamasishaji na andiko la mbio hizi”,amesema Mwalyambi.

Mwalyambi amesema maandalizi ya Mbio hizo yanaendelea vizuri na kwamba Mbio hizo zitafanyika Agosti 7,2022 wakati wa Kilele cha Maonesho ya Madini Mkoa wa Shinyanga.

“Tutakuwa na mbio za kilomita 21, 10, 5 na 2.5 kwa watoto pamoja na mbio za Baiskeli na michezo mbalimbali. Tunatarajia kuwa washiriki zaidi ya 1000 tunaomba wananchi wajitokeze kwa wingi kushiriki katika mbio hizi”,amesema.

Katika hatua nyingine amesema PJFCS inashirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kutembelea Vivutio vya Utalii na Utamaduni na upandaji miti.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema ameipongeza Klabu ya Mazoezi Police Jamii Fitness Center Shinyanga (PJFCS) kwa kuandaa Shinyanga Madini Marathon huku akiwashauri kushirikisha wadau kikamilifu mapema ili kufanikisha mbio hizo.

“Serikali ya Mkoa wa Shinyanga inaunga mkono Mbio hizi mlizoandaa. Tunataka Vibe! kweli kweli, hakikisheni mnajiandaa vizuri ili mbio hizi ziwe na tija. Hakikisheni mnashirikisha pia wasanii wa nyimbo za asili kwani wana wafuasi wengi ili mbio hizi ziwe za mfano..Ni matumaini yangu mtafanya vizuri”,amesema Mjema.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akiangalia Jezi ya uhamasishaji wa Shinyanga Madini Marathon 2022. Kushoto Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Shinyanga Madini Marathon, Roland Mwalyambi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Shinyanga Madini Marathon, Roland Mwalyambi (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema Jezi ya uhamasishaji wa Shinyanga Madini Marathon 2022.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Shinyanga Madini Marathon, Roland Mwalyambi akimwelezea Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema kuhusu Shinyanga Madini Marathon 2022.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Shinyanga Madini Marathon, Roland Mwalyambi (kulia) akimwelezea Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema kuhusu Shinyanga Madini Marathon 2022.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akisoma andiko kuhusu Shinyanga Madini Marathon 2022.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akisoma andiko kuhusu Shinyanga Madini Marathon 2022.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akizungumza na waandaaji wa Shinyanga Madini Marathon 2022
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akiwasisitiza waandaaji wa Shinyanga Madini Marathon 2022 kujiandaa kikamilifu.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akizungumza na waandaaji wa Shinyanga Madini Marathon 2022.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: