Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) leo Machi 8, 2022 imesaini mkataba na Kampuni ya Arqes Africa Architechs & Interior Designesers kwaajili ya kusanifu majengo ya Kituo cha Kikanda cha Umahiri wa Tehama (RAFIC) kazi ambayo inatakiwa kuanza mara moja na kukamilika ndani ya miezi minne.

Kazi ambazo anatakiwa kufanya mshauri elekezi huyo ni pamoja na kutengeneza 'Master Plan' ya DIT Kampasi Kuu ya Dar es Salaam, kusanifu majengo ya RAFIC na kumsimamia mkandarasi wakati wa ujenzi. Thamani ya kazi hiyo ni Sh 756,539,200

Hata hivyo Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam, Prof Preksedis Ndomba ameomba kazi hiyo ikiwezekana ikamilike ndani ya miezi miwili ili kupatikana kwa mkandarasi na kazi ya ujenzi ianze mara moja.

Katika tukio hilo la kusaini mkataba huo, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo, Arch. Lazaro Peter ameahidi kufanya kazi hiyo kwa umahiri mkubwa na ikiwezekana anajitahidi kukamilisha kazi ndani ya miezi miwili.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: