Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
WAKALA wa mabasi yaendayo haraka (DART ) kwasasa umeleta mabasi 19 ili kuboresha huduma ya usafiri Kibaha Mkoani Pwani,pamoja na kuanzisha ruti kuelekea hospital ya Tumbi kuwarahisishia usafiri watumishi na wagonjwa.
Kuanza kwa ruti hiyo kuelekea hospital ya Tumbi kutakomboa wakazi wa maeneo hayo, wagonjwa na watumishi waliokuwa wakipata kero kupanda bajaj ama pikipiki kwani hakuna usafiri wa uhakika wa mabus madogo.
Akielezea matarajio hayo ,wakati DART ilipotoa msaada wa vifaa vya afya na vitu mbalimbali hospital ya Tumbi ambapo Kaimu Mtendaji Mkuu DART, Mhandisi Dkt.Philemon Mzee alisema katika kuhakikisha wanatoa huduma bora wamejipanga kuongeza huduma zao Kibaha na Sasa mabus ya mwendokasi yanafika kila baada ya dakika tano,sita hadi Saba.
Mzee ambae pia ni kaimu mkurugenzi wa uendeshaji na usimamizi wa miundombinu alieleza,licha masuala ya usafirishaji,wanashirikiana na jamii kwenye mambo mbalimbali ikiwemo kusaidia mahitaji.
"Tumeshirikiana Leo na wenzetu Kampuni ya mabus yaendayo haraka UDART ,kutoa vifaa vya afya na vitu kwa wagonjwa ili kuunga mkono sherehe ya wanawake"
Mzee alitaja vifaa walivyotoa Kuwa Ni Pamoja na mashuka, sabuni,mafuta ya kupaka ,kiti Cha kubebea wagonjwa ,pempas na vifaa vya hospital vyote vimegharimu milioni mbili.
Nae Mkuu wa idara ya utawala na utumishi UDART, Zaitun Hassan alisema, mabus 19 yanafika Kibaha kila baada ya dakika tano Hadi Tisa na Lengo kufikisha huduma ya usafiri hadi Tumbi.
Kaimu mganga mkuu Tumbi, Dr. Silas Msangi alishukuru kwa msaada huo na kusema vifaa vilivyotolewa vitasaidia kuboresha huduma za kiafya.
Alisema Usafi wa mabus ya mwendo Kasi ukifika Tumbi utawasaidia watumishi na wagonjwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments: