Afisa Muuguzi wa Chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prisca Kiyuka akiwaelezea namna ambavyo wagonjwa wanapatiwa huduma katika chumba hicho madaktari kutoka Hospitali ya Ostrava iliyopo Jamhuri ya Watu wa Czech walipotembelea Taasisi hiyo kwa ajili ya kuona namna ambavyo wanaweza kushirikiana katika kutoa huduma za matibabu ya moyo jana Jijini Dar es Salaam
Fundi sanifu wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Kulindwa Kasubi akiwaelezea huduma ya upasuaji mdogo wa moyo inayotolewa katika chumba cha Cath Lab madaktari kutoka Hospitali ya Ostrava iliyopo Jamhuri ya Watu wa Czech walipotembelea Taasisi hiyo kwa ajili ya kuona namna ambavyo wanaweza kushirikiana katika kutoa huduma za matibabu ya moyo jana Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akijadiliana na madaktari kutoka Hospitali ya Ostrava iliyopo Jamhuri ya Watu wa Czech namna ambayo watashirikiana katika kutoa huduma za matibabu ya moyo jana baada ya madaktri hao kutembelea JKCI Jijini Dar es Salaam
Madaktari kutoka Hospitali ya Ostrava iliyopo nchini Czech na wenzao kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakifuatilia majadiliano wakati madaktari hao walipotembelea JKCI kwa ajili ya kuona namna ya kushirikiana katika kutoa huduma za matibabu ya moyo jana katika ukumbi wa Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi katika picha ya pamoja na madaktari kutoka Hospitali ya Ostrava iliyopo Jamhuri ya Watu wa Czech baada ya kufanya ziara katika taasisi hiyo kuona namna ambavyo wanaweza kushirikiana katika kutoa huduma za matibabu ya moyo jana Jijini Dar es Salaam. Picha na JKCI.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: