Chama cha mapinduzi Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa kimeipongeza Serikali ya awamu ya sita kwa kufanikisha miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo ya Maji uboreshwaji wa miundombinu ya barabara, Afya na elimu.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kilolo Kiliani Myenzi alisema Serikali imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutekeleza kwa vitendo ahadi za maendeleo kwa wananchi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani na kuchochea maendeleo.
Kiliani Myenzi ameyasema hayo wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 45 ya CCM wilayani humo na kuwahimiza wananchi kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuboresha maisha ya watanzania kupitia miradi ya maendeleo.
Alisema kwa kipindi kifupi ambacho Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameingia madarakani amefanikiwa kuboresha kila sekta kwa ajili ya kukuza uchumi wa wananchi na kuiletea maendeleo wanananchi.
Myenzi
alisema kuwa wananchi wa wilaya ya kilolo mkoani Iringa wanamuunga mkono Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kazi
anazozifanya na wapo tayari kumpigania tena mwaka 2025 kwenye uchaguzi mkuu.
Aliesma kwa upande wa wilaya ya Kilolo amepeleka fedha nyingi kutatua kero ya ya Maji uboreshwaji wa miundombinu ya barabara, Afya na elimu na sasa wananchi wanafura na uongozi wake.
Nao baadhi ya wananchama wa chama cha mapinduzi wilaya ya Kilolo walisema kuwa wanaunga mkono kinachofanywa na mwenyekiti wa chama hicho ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ya keleta maendeleo kwa watanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments: