Pichani ni sehemu ya Zawadi zilizotolewa na Wananchi wa Kijiji Butainamwa Kama shukrani zao kwa Wafadhili kwa kuwajengea Shule Mpya. (Picha zote na Dulla Uwezo)
Na Abdullatif Yunus - Michuzi TV.

Changamoto ya Uhaba wa Walimu Katika Shule ya Msingi iliopo Kata Kasharu Halmashauri ya Wilaya Bukoba, bado imeendelea kuwa Kizungumkuti, licha ya Shule hiyo kuboreshwa miundo mbinu upya ya Madarasa na Matundu ya Vyoo.

Hayo yamebainika katika hafla ya makabidhiano ya Majengo mapya ya Madarasa Saba pamoja na Matundu Tisa ya Vyoo vya Shule hiyo, yaliyofadhiliwa na Jamhuri ya Watu wa Korea kupitia Shirika lao la GRORY REACH AND HELP FOUNDATION lenye Makao Makuu yake Jijini Arusha, hafla iliyofanyika Shuleni Butainamwa Novemba 08, 2021.

Akisoma Risala Mkuu wa Shule ya Butainamwa Mwl. Venant Byabato kwa Mgeni Rasmi Ndg. Fatina Laay Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Bukoba, amebainisha upungufu wa Walimu Katika Shule hiyo ambayo Ina jumla ya Wanafunzi 468 ikiwa na Walimu wanne wa kiume na mmoja wa kike, jumla Walimu Watano suala linapolekea kushuka kwa Taaluma.

Aidha Mwl. Venant mbali na shukrani alizoziwaailisha kwa Wahisani hao, amezitaja changamoto nyingine katika Shule hiyo kuwa Ni Maji, Umeme, Lishe kwa Wanafunzi pamoja na Ofisi ya Walimu. Shule hiyo imejengwa Tena upya na Wafadhili (Wakorea) hao kwa kipindi cha Miezi mitatu ambao waliofika Kijini Butainamwa kwa Shughuli na Huduma za kiroho na kuona hitaji hilo kwa wananchi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Bukoba Bi. Fatina Laay akikabidhi kwa niaba ya Serikali, cheti cha utambuzi kwa Wafadhili kufuatia Jambo walilofanya kwa WanaButainamwa.
Mkuu wa Shule ya Msingi Butainamwa Mwl. Venant Byabato akisoma Taarifa ya shule ya Msingi Butainamwa wakati wa Makabidhiano ya majengo mapya ya Shule hiyo.
Muonekano wa Majengo mapya ya Shule ya Msingi Butainamwa yaliyojengwa na Wafadhili kutoka Nchini Korea.
Muonekano wa Jengo jipya la Matundu Tisa ya Vyoo katika Shule ya Msingi Butainamwa lililojengwa kwa ufadhili wa Wakorea.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: