Mkurugenzi wa Mazingira na Usalama katika Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Idara ya Usafiri wa Usalama wa Mazingira ya Usafiri nchini na Mwenyekiti wa Mkutano wa wadau wa kupokea maoni ya kanuni za wakala wa Meli na Forodha Stella Katondo akizungumza wakati wa mkutano wa wadau hao leo Jijini Tanga kulia ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TASAC ambaye pia ni Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumi wa TASAC Nahson Sigalla na kushoto ni Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Timotheo Sosiy
Mkutano wa wadau wa kupokea maoni ya kanuni za wakala wa Meli na Forodha ukiandelea kwenye Ukumbi wa Bandari Jijini Tanga leo
Wadau wakifuatilia mkutano wa wadau wa kupokea maoni ya kanuni za wakala wa Meli na Forodha leo uliofanyika kwenye ukumbi wa Bandari Jijini Tanga
MKUTANO wa Wadau wa kupokea maoni ya kanuni za Wakala wa Meli na Forodha umefanyika leo mkoani Tanga ukihusisha wadau wa usafi kwa njia ya maji ikiwemo Bahari na Maziwa ambao ulijadili mapendekezo ya kanuni mpya za watendakazi wanaosimamiwa na Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC).
Akizungumza katika mkutano huo Mwenyekiti wake ambaye ni Mkurugenzi wa Mazingira na Usalama katika Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na hususani Idara ya Usafiri wa Usalama wa Mazingira ya Usafiri nchini Stella Katondo ambapo alisema wamewakutanisha wadau hao ili kujadili mapendekezo ya kanuni mpya katika kuanzisha kanuni za Benchmark za wale watenda kazi wanaosimamiwa na Shirika la TASAC.
Alisema kwamba wanataka wawe na vigezo vya upimaji watendaji kazi wao na wamepeleka mapendekezo hayo na watayapokea maoni kutoka kwao ambao wanashiriki kwenye kazi hizo ili waweze kuyaweka kwenye kanuni ili pale wanapofanya kazi waweze kuwa wamepimwa watatekeleza kazi hizo hasa kule chini kwa walaji ambao watakuwa wanapata huduma ambazo wanazitoa.
Aliwataja watendaji hao ni Wakala wa Forodha,Clearing and Forwarders na wenye meli na wote wanaohusika kwenye tasnia hiyo ili kuweza kuanzisha hizo kanuni ambazo zitawasaidia wakati wanapokuwa wakitumiza wajibu wao.
“Kumekuwa na mapendekezo ya marekebisho kwenye kanunuzi hizo kanuni zilikuwa tayari hivyo hivi sasa tunatarajia kuzirekebisha ziendane ma mazingira yatakayohusisha upamaji wa utendaji kwa ufupi ni hivyo tupo mkoani Tanga kwa ajili ya kuendelea kupata maoni kwa wadau”Alisema
Mkurugenzi huyo wa Mazingira na Usalama Uchukuzi alisema japo kumekuwa na ushirikishwaji kwenye maeneo ya maziwa makuu walikuwa hawajashirikishwa katika zile kanuni za awali kwa kwenye mapendekezo hayo mapya.
“ Hivyo ndio maana leo kwenye vikao vya wadau vinaendelea Mwanza kwa kuwashirikisha wadau maeneo hayo kwani Shirikia la Meli sio linafanya kazi kwenye mwambao wa bahari tu bali hata kusimamia watendaji kazi waliopo kwenye maziwa makuu”Alisema
Ambayo yanaendesha huduma za usafirishaji kwa njia ya maji kwa meli hicho ni kipengele ambacho kimekumbukwa na kimepelekwa kwa wadau kusubiri waweze kutoa mapendekezo yao ili kuiingizwe katika kanuni ambazo zinatarajia kusimamia utendaji kazi.
“Katika kanuni hizo wametoa nafasi kwa wadau kwanza waweze kutoa mapendekezo na hatimaye kiingizwe kwenye kanuni,wamepewa nafasi kwanza wadau wamepeleka mapendezo yao yatapokelewa na sekratarieti kwani ni mchakato hivyo bado wana nafasi ya kupokea maoni.
Awali akizungumza katika mkutano huo Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC) Nason Sigala alisema kinachofanyika katika mkutano huo ni ukusanyaji wa kupokea maoni kutoka kwa watumiaji,wadau katika sekta ya usafiri na usafirishaji wa majini.
Alisema zoezi hilo la upokeaji wa maoni ya mapendekezo ya kanuni mpya za vigezo vya utendaji na marejeo ya marekebisho ya kanuni ya wakala wa mali ni mchakato ambao unataratibiwa na wizara ya Ujenzi na Uchukuzi sehemu ya uchukuzi.
Sigalla ambaye ni Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumi wa TASAC alisema wao kama Shirika la Wakala wa Meli Tanzania(TASAC) wameshiriki kwenye vikao hivyo kama wadau muhimu baada ya kanunu hizo kupitishwa wao watahusika moja kwa moja kama msimamizi katika utekelezaji hivyo matarajio yao baada ya kanunuzi hizo kupiti kwa kiasi kikubwa ufanisi na ubora wa huduma zinazodhibitiwa utaimarika kwa kiwango kikubwa.
Naye kwa upande wake mmoja washiriki kwenye mkutano huo kutoka Kampuni ya CMA Shiping Line Lucy Jackson alisema marekebisho ya kanuni ambazo wameelezewa vitawasaidia wadau wanaotumia bandari kunufaika kwa sababu zimefanyiwa marekebisho na kukidhi mahitaji ya wateja.
Lucy alisema kabla ya kununi hizo kupendekeza zilikuwa zinawaathiri katika utendaji wa kazi nyakati tofauti tofauti kwa sababu unakuta kanuni hazijabezi kwa watumaji wa bandari kwa hiyo marekebisho yameangalia ni athari gani walikuwa wanazipata.
Alisema baada ya marekebisho hayo wanategemea watanufaika huku akieleza kwamba ilikuwa inawaadhiri kwa upande wa Shiping Line kwa sababu unakuta wateja wao ambao ni wadau wakubwa wanaohusiana na makasha hawajui hizo sheria hivyo namna ya kuwaelezea inakuwa vigumu.
Toa Maoni Yako:
0 comments: