Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Seleman Jofo akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kisarawe Ushoroba Festival leo Machi 5, mwaka huu.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani,Jokate Mwegelo(katikati)akichezo ngoma ya asili ya kabila la Wazaramo leo Machi 5,2021 wakati wa uzinduzi wa tamasha la Kisarawe Ushoroba Festival ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Seleman Jafo.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani Jokate Mwegelo akizungumza mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo wakati wa uzinduzi wa Kisarawe Ushoroba Festival.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Selemani Jafo akiwa katika meza kuu wakati wa uzinduzi wa tamasha hilo uliofanyika leo wilayani Kisarawe.
Mwakilishi wa Shirika la Bima la Taifa akizungumza wakati wa uzinduzi wa tamasha Kisarawe Ushoroba Festival leo Machi 5,2021.
Na Said Mwishehe, Michuzi TV
KUMEKUCHA Kisarawe! Ndivyo unavyoweza kuelezea baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Seleman Jafo kuzindua rasmi Kisarawe Ushoroba Festival huku akiwataka wadau kuchangamkia fursa mbalimbali zitakazozalishwa kutokana na utalii uliopo ndani ya wilaya hiyo.
Akizugumza leo Machi 5,2021 wakati akizundua tamasha la Kisarawe Ushoroba Festival ambapo wadau mbalimbali wameshiriki , Waziri Jafo amesema kwanza anatoa shukrani kwa Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dk.Aloyce Nzuki kwa uamuzi wake wa tamasha hilo kuliweka kwenye ya utalii ili inapokaribia tarehe kama ya leo kwa kila mwaka watalii wawe wanakwenda Kisarawe kushiriki tamasha hilo.
"Nakushukuru sana Katibu Mkuu (Nzuki) kwa kusema tukio hilo litawekwa kwenye kalenda ya matukio utalii ya mwaka na kuwataka wadau wa uwekezaji kuiona hatua hiyo kuwa fursa hivyo waichangamkie.Wawekezaji sasa njooni muanze kuwekeza Kisarawe ili kuweza kuwahudumia wageni na kuzalisha ajira,"amwesema Waziri Jafo.
Aidha amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo kwa ubunifu mbalimbali unaoendelea kuiletea tija Kisarawe huku akiahidi kushirikina na Serikali ya Wilaya wataendelea kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo.
Awali Dk.Nzuki wakati anazungumzia tamasha hilo ameeleza Wizara yake imeguswa na ubunifu uliofanywa na Wilaya ya Kisarawe kuanzisha tukio la Kisarawe Ushoroba Festival, na wataangali uwezekano wa kuliingia katika kalenda ya matukio ya utalii ynayotambuliwa na wizara yake.
Akifafanua kuhusu tamasha hilo ambalo litafanyika kwa siku tatu kuanzia leo,Dk. Nzuki amesisitiza tamasha hilo limepewa jina muhimu la ushoroba ambalo ni muhimu katika sekta ya uhifadhi na utalii, kwa kuwa linatao hamasa ya kutunza 'shoroba' (maeneo ya mapito ya wanyma).
Ameongeza kunmekuwapo na changamoto kwa wananchi kukaa kwenye shoroba, hivyo kusababisha madhara mbalimbali ikiwamo kushambuliwa na wanyamapori.
Aidha amesema tamasha hilo ni muhimu kwani linatengeneza matukio muhimu ya utalii na kuhamasisha uhifadhi na utalii jambo ambalo linastahili kuwekwa katika kalenda ya wizara ya matukio ya utalii nchini."Tunampongeza DC (Mkuu wa Wilaya) Kisarawe, Jokate Mwegelo kwa ubunifu na tunaahidi kukuunga mkono.
"Wizara ya maliasili ipo pamoja na wilaya ya kisarawe na tutaendelea kuunga mkono kuhakikisha tunafungua fursa mbalimbali zitokanazo na utalii," Dk.Nzuki amesisitiza wakati akielezea umuhimu wa tukio hilo.
Akizungumza wakati akiwakaribisha wageni waliohudhuria uzinduzi wa tamasha hilo Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo amesema jambo hilo walianza kuliwaza tangu mwaka 2018 na sasa wanashukuru kwa kuona limetimia."Tunawashukuru wadau wote walioguswa na leo hii kuitikia na kuhudhuria shughuli hii.
"Tunaomba huu usiwe mwisho bali uchukuliwe kama mwanzo wa kutuunga mkono kwa hatu kubwa zaidi hapo baadae.Nawaomba wananchi na wawekezaji kutumia fursa za uwekezaji kwa kuwa wanaamini Kisarawe itakuwa ikipokea wageni wengi wanaokuja kwa ajili ya utalii,"amesema.
Ameongeza wanaendelea na miradi mbalimbali ili kutoa fursa kwa vijana kwa kuwa hatutaki kuona vijana wakikaa Vijibweni."Tamasha hili litakuwa la siku tatu likiwa na matukio mbalimbali ikiwamo kutembelea maeneo ya vivutuo vya utalii.
"Mbio za marathon na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali.Tunataka kuutangaza utalii wetu pamoja na kuzungumzia uwekezaji , kwani tunayo maeneo mazuri kwa kuwekeza , karibu wadau wote mje kuwekeza ndani ya Wilaya ya Kisarawe,"amesema Jokate.
Toa Maoni Yako:
0 comments: