Mkuu wa Shule ya Kibaha Sekondari, Mwl. Chrisdom Ambikile (wapili kulia) akitoa ufafanuzi mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa pale kamati hiyo ilipokagua Maabara ya Shule ya Sekondari Kibaha leo Mkoani Pwani. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Humphrey Polepole

Wajumbe Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, wakikagua sehemu ya kunawia mikono kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kibaha ikiwa sehemu ya Mradi wa Maendeleo Shuleni hapo tukio lililofanyika leo Mkoani Pwani.


Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. David Silinde akitoa ufafanuzi wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa ilipotembelea na kukagua Matumizi ya Mfumo wa TEHAMA (GoTHOMIS) katika usimamizi na uendeshaji wa hospitali ya Rufaa ya Tumbi ya Mkoa wa Pwani.


Wajumbe kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, wakikagua kisima cha Maji ikiwa ni mmoja ya Miradi ya mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) inayotekelezwa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika Mkoa wa Pwani.


Wajumbe kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, wakikagua Bwawa la Maji ikiwa ni mmoja ya Miradi ya mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) inayotekelezwa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika Mkoa wa Pwani.

Mkurugenzi wa Shirika la Elimu Kibaha, Ndg. Robert Shilingi (katikati) akizungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Humphrey Polepole (wapili kushoto) pale kamati hiyo ilipowasili ili kutembelea na kukagua Miradi ya Maendeleo ya Shule ya Sekondari Kibaha leo Mkoani Pwani. Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: