Ofisa Mauzo Ezekiel Kwaka (kulia), akitoa maelezo kuhusu ubora wa Mkaa Mweupe wakati wa Maonesho ya Wakulima ya Nanenane Kanda ya Kati kwenye viwanja vya Nzuguni, jijini Dodoma yaliyomalizika hivi karibuni. Mkaa huo ambao ni rafiki wa mazingira ulikuwa unauzwa kwenye mifuko sh.3000 na 5000 na 20000 kutokana na wingi wa vipande vya mkaa.
Vipande vya Mkaa Mweupe vidogo na vikubwa ambapo vidogo hutumika kwa majiko madogo na vikubwa kwa majiko makubwa.
Aristotle Nikitas Meneja Masoko wa Kampuni ya Premium Active Tanzania Limited, inayotengeneza Mkaa Mweupe, akipokea cheti kutoka kwa Mkuu wa Mkoa Singida, Dk. Rehema Nchimbi baada ya kampuni hiyo kuibuka mshindi wa pili kundi la Wajasiriamali na Wawekezaji wadogo wakati wa kilele cha Maonesho ya Wakulima ya Nanenane Kanda ya Kati kwenye viwanja vya Nzuguni, Dodoma.
Wananchi wakisikiliza kwa makini wakati Ofisa Mauzo, Ezekiel Kwaka akielezea kuhusu matumizi ya vipande vidogo vya mkaa ambapo alisema kati ya vipande vitatu au vinne kupika vyakula kwa takribani masaa manne bila kuzimika. Mfuko mmoja wenye vipande vidogo 30 huuzwa sh.3000.
Jiko kubwa linalotumia vipande vikubwa vya Mkaa Mweupe ambalo lilikuwa linaoneshwa jinsi mkaa huo unavyoivisha kande. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Toa Maoni Yako:
0 comments: