NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso akizungumza wakati akifungua mkutano wa wadau wa mamlaka ya Maji na Usafiri wa Mazingira (Tanga Uwasa) wilaya ya Pangani kulia Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly
KATIBU Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassan Nyange kulia akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo kushoto ni Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly akifuatiwa na Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo
MENEJA Ufundi wa Tanga Uwasa Mhandisi Rashid Shabani akieleza mkakati wa kuboresha huduma za maji mjini Pangani wakati wa mkutano huo
Kaimu Mkuu wa kitengo cha Huduma kwa Wateja Rogers Machaku
Meza kuu wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye mkutano huo wa wadau
MKURUGENZI wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani Isaya Mbenje akiwa kwenye meza kuu na Mwenyekiti wa mkutano huo wa wadau kulia na wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly
NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso kushoto akisalimiana na MENEJA Ufundi wa Tanga Uwasa Mhandisi Rashid Shabani wakati alipowasili kufungua mkutano huo katikati ni Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly
Sehemu ya wananchi wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye mkutano huo wa wadau
Mmoja wa wananchi akiuliza swali katika mkutano huo
Sehemu ya wadau mbalimbali wakifuatilia mkutano huo
Sehemu ya wadau mbalimbali wakifuatilia mkutano huo
Sehemu ya wadau mbalimbali wakifuatilia mkutano huo
NAIBU WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso ameziagiza mamlaka za maji nchini kuwa na utaratibu wa kuwashirikisha wadau wanaotumia huduma za maji kwenye maeneo yao.

Aweso aliyasema hayo wakati akifungua mkutano wa wadau wa mamlaka ya Maji na Usafiri wa Mazingira (Tanga Uwasa) wilaya ya Pangani ambapo alisema ni muhimu wadau kushirikishwa.

Alisema hilo linatokana na kwamba wao ni muhimu na ndio wenye maeneo yao hivyo ni wajibu kuona namna ya kuwashirikisha badala ya kwenda tu bila wao kutambua.

Aidha aliwapongeza Tanga Uwasa kwa kuwashirikisha wahusika kwani moja ya makosa makubwa yanayofanywa na wataalamu wetu licha ya kuwa na elimu kubwa lakini kosa kubwa wanalolifanya ni kutokuwashirikisha wahusika.

“Ndugu zangu mtambue kwamba anayelala na mgonjwa ndio anayejua muhimo yake leo mnaweza kuja na magari na vifaa bila kuwashirikisha wadau mnaficha nini?...niwaombe mshirikiana na hao viongozi hamtashindwa chochote kwani hata leo pakitokea ubadhirifu watawapa taarifa “Alisema Naibu Waziri huyo.

“Leo huu ni mkutano wa wadau wa Tanga Uwasa Pangani niwapongeze Tanga Uwasa kwa hatua hii muhimu lakini nitoe agizo kwa mamlaka za maji nchini kuwa na utaratibu wa kuwashirikisha wadau wanaotumia huduma ya maji kwenye maeneo yenu kwani wao ndio wenye maeneo yao na na sio kwenda tu “Alisema Naibu Waziri Aweso.

Akizungumzia suala la bili za maji, Naibu Waziri Aweso alisema ni wajibu na jukumu la wananchi kupatiwa maji na mwenye jukumu hilo ni wizara ya maji kupitia mamlaka za maji.

Alisema pamoja na jukumu hilo lakini wasisahau kwamba wananchi wana wajibu wa kuhakikisha wanalipa bili za maji lakini zisiwe bandikizi ambazo zitaleta manung’uniko kwao

“Kwamba kama mtu leo anatumia maji ya elfu thelathini unamuambia alipe laki mbili kama anakiwanda na ndio maana tukatoa agizo kwamba mnaposoma bila za maji muwashirikishe wananchi husika”Alisema Naibu Waziri Aweso.

Pia alisema wizara hiyo imefanya maboresho makubwa wanajua mji wa Pangani watu wameongezeka ukilinganisha na kipindi cha nyuma tumepata mradi wa milioni 500 umetengenezwa wananchi wanapata maji .

Hata hivyo alisema yeye kama Mbunge wa Pangani kilio chake cha muda mrefu ni kuona kwanini Mto pangani unapita katikati ya mji wa Pangani lakini haya maji hayatumiki hicho ndio kilio kweli muosha huoshwa.

“Mh Rais akanipa Wizara ya Maji naomba nizungumze kwa heshima na ujasiri mkubwa tenda zaidi ya miji 24 miradi mikubwa na sisi Pangani tutatumia maji ya Mto Pangani lakini utakwenda pia miji ya Muheza na Handeni na Korogwe hata nikifa leo hii kumbukumbu haitasahauilika kwa kazi kubwa aliyoifanya Rais wetu”Alisema Naibu Waziri huyo.

Hata hivyo alisema kwamba mamlaka ya Maji ya Tanga Uwasa wamekuwa wakifanya vizuri sana kila mwaka na ndio maana wakaona wawaunganishie na wilaya za Muheza na Pangani.

Awali akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga “Tanga Uwasa” Mhandisi Geofrey Hilly alisema leo wapo Pangani kuongea na wadau wao mbalimbali kwa ajili ya kuweka uelewa mpana kwanini wao wa Tanga Uwasa wamekwenda kutoa huduma kwenye mji huo . 

Alisema kwamba mji wa Pangani utaratibu wa sasa una kata nne una wakazi wapatao 19100 ambao wanapaswa kuwahudumia kwa hiyo wamepata viongozi wa ngazi ya chini mpaka juu kuongea nao na wakiongea nao ni sawa na kuwafikia wananchi.

Alisema wajue kwamba kwa nini Tanga Uwasa wanatoa huduma huko huku akieleza hayo ni maamuzi ya Serikali kupitia Rais Dkt John Magufuli ambapo mwaka 2017 alitangaza rasmi huduma za maji zote zisimamiwe wizara ya maji.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: