Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe.Jamhuri William akikabidhiwa madawati na Kaimu Meneja wa Shamba la Miti SaoHill Bw.Daniel Silima katika makabidhiano ambayo yaliyofanyika katika Shule ya Msingi Mbalwe.

Na Mwandishi Wetu.

Wakala Wa Huduma za Misitu Tanzania kupitia Shamba la Miti SaoHill limekabidhi madawati katika Shule ya Msingi Mbalwe iliyopo katika Kijiji cha Wami Mbalwe Wilayani Mufindi.

Madawati hayo yamekabidhiwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. David Willium kwa niaba ya Shule hiyo ikiwa ni sehemu ya kuchangia shughuli za maendeleo katika vijiji vinavyolizunguka shamba.

Akizungumza wakati wa kukabidhiwa madawati hayo Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri William amesema kuwa anaipongeza TFS kupitia Shamba la Miti SaoHill kwa jitihada wanazozionesha kwa kushirikiana na jamii kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo Wilayani.

“Nawapongeza sana SaoHill kwa kuwa majirani wazuri wa wananchi, mmetuchangia madawati 30 lakini bado tuna mahitaji ya madawati sehemu nyingine endeleeni kutusaidia”. Amesema Mhe. Jamhuri William

Ameongeza kuwa anatoa wito kwa wadau wengine Wilayani kuendelea kuchangia shughuli za maendeleo na hivyo viongozi katika maeneo husika kuhakikisha wanasimamia vyema maendeleo hayo.

Aidha Kaimu Meneja wa Shamba la Miti SaoHill Bw. Daniel Silima amesema kuwa ugawaji wa madawati haya 30 ni sehemu tu ya jitihada za kuonyesha ushirikiano katika jamii inayolizunguka shamba.

Alisema Bw. Daniel Silima “Hii ni sehemu ya kurejesha fadhira kwa jamii ambayo inazunguka shamba kwani wamekuwa ni sehemu kubwa katika ulinzi wa misitu katika Wilaya ya hii ya Mufindi.

Hadi sasa TFS kupitia Shamba la Miti SaoHill limetoa madawati zaidi ya 1,000 katika jamii inayolizunguka shamba ikiwa ni pamoja na nje ya Wilaya ya Mufindi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: