Timu ya Aston Villa FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza EPL imekamilisha usajili wa mchezaji wa kimatafa kutoka timu ya KRC Genk ya Ubeligiji na timu ya taifa ya Tanzania Mtanzania Mbwana Ali Samata mwenye umri wa miaka 27.

Mbwana Samata amesaini mkataba wa kuitumikia klabu hiyo kwa miaka minne na nusu 2020-2024 kuanzia jana kwa kitita cha Paundi milioni 10.

Watanzania kote duniani walikuwa wakisubiri kwa hamu usajili huo ambao unamletea mafanikio na sifa mtanzania huyo na kuipa sifa Tanzania katika anga za mchezo wa mpira wa miguu.

Akizungumzia usajili huo Meneja wa Klabu hiyo Dean Smith amesema tumefanikiwa kumleta Mbwana Samatta katika klabu yetu.

Ameongeza kuwa Mbwana Samatta atakuwa mchezaji wa kwanza kutoka nchini Tanzania kucheza Ligi Kuu ya Uingereza EPL lakini hatakuwepo wakati Aston Villa itakapocheza katika uwanja wa nyumbani na timu ya Watford Jumanne.

Mbwana Samatta akiichezea KRC Genk misimu minne aliifungia klabu hiyo magoli 43 katika michuano mbalimbali likiwemo goli maridadi kabisa alilofunga kwa kichwa wakati KRC Genk ilipoifunga timu ya Liverpool katika michuano ya klabu bingwa Ulaya kwenye mchezo wa marudiano uliochezwa Uingereza katika uwanja wa Liverpool.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: