Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu (katikati) akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Makungu Wilaya ya Ikungi mkoani Singida juzi,  wakati akikagua mradi wa maji waliowezeshwa na Rais John Magufuli.
 Mbunge Kingu akiwahutubia wananchi hao katika mkutano wa hadhara.
 Katibu Muenezi na Itikadi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Iyumbu, Lameck Maguni akizungumza kwenye mkutano huo.
 Wananchi wa Kijiji cha Iyumbu wakiwa kwenye mkutano.
 Katibu wa CCM Kata ya Iyumbu, Mohammed Itambu akizungumza.
 Mbunge Kingu akiserebuka katika mkutano huo.
 Mwenyekiti wa CCM Tawi la Makungu, Weja Ng'waya akizungumza.
 Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Kata ya Iyumbu, Njile Gasamalu akizungumza.
 Diwani wa Kata ya Iyumbu, Peter Gwiligwa akizungumza.
 Mwenyekiti wa CCM Kata ya Iyumbu, Juma Okumu akizungumza.
 Wananchi wa Kijiji cha Iyumbu wakiwa kwenye mkutano.
Kingu akiwahamasisha wananchi kwenda kujiandikisha.

Na Dotto Mwaibale, Singida

WANANCHI wa Kijiji cha Makungu Kata ya Iyumbu Wilaya ya Ikungi mkoani Singida wamemshukuru Rais John Magufuli na Mbunge wao Elibariki Kingu kwa kuwachimbia kisima cha 
maji.

Shukurani hizo walizitoa juzi katika mkutano wa hadhara aliouandaa mbunge huyo wakati akikagua miradi ya maendeleo pamoja na kuwahamasisha kujiandikisha kwa wingi ili waweze kuwachagua viongozi wa vijiji, vitongoji kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Mwishoni mwa mwaka jana wananchi hao walizuia msafara wa mbunge huyo na kumuonesha mabango yenye kero mbalimbali kubwa ikiwa ni kukosa maji ambapo aliipeleka kwa Rais Magufuli ambaye amewachimbia kisima hicho ambacho kitasambaza maji katika kijiji hicho na vitongoji vingine vya jirani.

Kingu alisema wanamshuru Rais John Magufuli kwa kusikia kilio chao hivyo kutokana na heshima hiyo aliowapa watahakikisha  viongozi wote katika uchaguzi wa serikali za mitaa vijiji na vitongoji wanatoka Chama Cha Mapinduzi (CCM)

" Ndugu wananchi heshima pekee ya kumshukuru Rais wetu kwa kutuletea mradi huu wa maji ni  kuhakikisha tunakipa ushindi mkubwa chama chetu naombeni twendeni tukajiandikishe kwa wingi na siku ikifika ya kupiga kura basi tuwachague viongozi watakaounda serikali kupitia CCM" alisema Kingu.

Alisema serikali imewapendelea sana Jimbo la Singida Magharibi kwa kuwapelekea miradi ya  maji 24 na sasa hivi kuna magari mawili yenye mitambo ya kuchimba maji yapo maeneo mbalimbali ya jimbo hilo ambapo katika kijiji hicho maji yaliyopatikana yatakuwa yakitoka lita 11,000 kwa saa na kuwa sh.350 milioni zimetengwa kwa ajili ya miundo mbinu ya kusambaza maji kwenye kijiji hicho na kufunga DP.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: