Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mhe. Regina Chonjo akizungumza na madiwani, watendaji wa halmashauri za Kinondoni na Morogoro walipokuja kwenye ziara ya kujifunza namna ya ukusanyaji mapato. Wa kwanza kushoto ni Mstahiki Meya wa Morogoro Amir Nondo na Mstahiki Meya Benjamini Sita wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni na Katibu Tawala Wilaya ya Kinondoni, Bi.Stela Msofe.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro. Mhe. Regina Chonjo akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika mradi mkubwa wa soko la kisasa lililopo magomeni.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo akizungumza na madiwani , watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro walipofanyaziara jana kwa lengo la kujinza namna ya ukusanyaji mapato. Wengine ni Meya wa Halmashauri ya Morogoro wa kwanza kushoto Amir Nondo na wapili ni Benjamini Sita.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, ambaye ni Mkuu wa Idara ya Mipango miji na Ardhi Kazi Maduhu akizungumza na watendaji , madiwani wa Halmashauri ya Morogoro na Kinondoni jana. Wa kwanza kulia ni Naibu Meya George Manyama.
Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro wakifuatilia uwasilishwaji wa namna ya ukusanyaji mapato.
Mstahiki Meya wa Halmsahauri ya Manispaa ya Kinondoni, Mhe. Benjamini Sita (wapili kushoto)Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Morogoro Amir Nondo (wakwanza kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Morogoro mjini Mhe. Regina Chonjo (wapili kulia) na Katibu Tawala wa Kinondoni Bi Stela Msofe wakiskiliza maoni mbalimbali kutoka kwa waheshimiwa madiwani.
Msimamizi wa Mapato wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Zahoro Rashidi akiwasilisha taarifa ya namna ya ukusanyaji mapato mbele ya madiwani , watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.
Picha ya pamoja.
Afisa biashara wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Pastor akiwaelekeza jambo madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kuhusu mradi wa Soko la Kisasa la Magomeni.
Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro jana walifanya ziara ya kujifunza namna ya ukusanyaji mapato katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.
Madiwani hao waliokuwa wameambata na Mkuu wa Wilaya hiyo Mh. Regina Chonjo, Mstahiki Meya Amir Nondo wamepokelewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Aron Kagurumjuli, Mstahiki Meya Benjamini Sita.
Aidha madiwani hao pia wamepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo , Katibu Tawala Stela Msofe pamoja na watumishi wengine wa Idara na vitengo ambapo pamoja na mambo mengine walipata nafasi ya kutembelea miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo Soko la Kisasa la Magomeni linalojengwa kwa shilingi bilioni 8.9.
Awali kabla ya kutembelea miradi hiyo , madiwani hao walipata nafasi ya kujifunza mbinu mbalimbali za ukusanyaji wa mapato zilizotolewa na Msimamizi wa Mapato wa Halmashauri ya Kinondoni Zahoro Rashidi.
Akizungumzia ziara hiyo, Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Morogoro Mhe. Nondo alisema kuwa wamekuja kujifunza namna ya ukusanyaji wa mapato kwakuwa Halmahauri ya Kinondoni imekuwa ikifanya vizuri kwenye ukusanyaji.
“ Tumekuja kujifunza namna ya ukusanyaji mapato, ukiangalia kwenye takwimu zetu sisi tuponyuma, sasa leo tumekuja kuona wenzetu mnafanyaje hadi mnafikia malengo, wote ni wamoja tunategemeana ,tunaomba mtupatie ujuzi mliokuwa nao” alisema Mhe. Nondo.
Kwaupande wake Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Chonjo alisema aliishukuru Manispaa ya Kinondoni kwakuwapokea vizuri na kueleza kuwa wamefurahishwa na ukarimu waliopata kutoka kwa viongozi na watendaji wa Halmashauri hiyo.
“ Lengo letu na kuja hapa ni kujifunza, tunawshukuru mmetukaribisha , undugu tuliouanzisha hapa isiwe mwisho, karibuni na nyinyi Morogoro, hili tunalolifanya ndio lile linalotakiwa na Rais Dk. John Magufuli, asanteni kwa ushiikiano wenu” alisema Mhe. Chonjo.
Akiwakaribisha Madiwani hao, Mstahiki Meya . Mhe. Sita alisema kuwa Halmashauri ya Kinondoni ipo vizuri kwenye ukusanyaji wa mapato na kwamba anawakaribisha ili waweze kujinza kwa lengo la kutimiza adhma hiyo.
Naye Mhe. Chongolo ambaye ni Mkuu wa Wilaya hiyo alisema kuwa ilikufikia malengo ,viongozi hawana budi kuweka juhudi nania ya dhati katika kutekeleza majukumu yao na kwamba kila mmoja anapaswa kushiriki kikamilifu katika kutekeleza wajibu wake.
“ Bila kuweka malengo ya dhati kabisa, tunaweza kufanya ziara za kujifunza tukamaliza maeneo yote, natusipae kitu, kikubwa ni kuweka nia, kama ilivyo kwa wenzetu wa kabila la hehe wakisema wanajinyonga basi wanajinyonga kweli, inamana waliweka nia , kwahiyo nasisi viongozi tuwaige wahehe katika kuweka nia ya kuleta maendeleo.
Toa Maoni Yako:
0 comments: