Mkurugenzi Mtendaji wa Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE), Dkt. Aggrey Mlimuka, akitoa hotuba ya ufunguzi wa mafunzo kuusu masuala ya Fidia kwa Wafanyakazi yaliyotolewa kwa Waajiri kutoka sehemu mbalimbali nchini na kufanyika jijini Dar es Salaam Novemba 28, 2019.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE), Dkt. Aggrey Mlimuka (kushoto), akisalimiana na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omary, mara baada ya kutoa hotuba.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omary, akizungumza mwanzoni mwa mafunzo ya siku moja kuhusu masuala ya Fidia kwa Wafanyakazi kwa wanachama wa Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) jijini Dar es Salaam Novemba 28, 2019.
Bw, Deo Ngowi kutoka kitengo cha Sheria Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), akiwasilisha mada kuhusu Sheria iliyoanzisha Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi.
Bw.Pascal Rischard kutoka Kitengo cha Usajili na Uwasilishaji Michango WCF, akiwasilisha mada kuhusu namna ya kujisajili na kuwasilisha michango kupitia Portal ya WCF
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omary,
Meneja Madai Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bi. Rehema Kabongo, akiwasilisha mada kuhusu Mafao yatolewayo na WCF.
Bw. Mihayo Mathayo, kutoka kitengo cha IT Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), akitoa mada ya namna ya kupata huduma mbalimbali za Mfuko kupitia mtandao.
Bw. Mihayo Mathayo, kutoka kitengo cha IT Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), akitoa mada ya namna ya kupata huduma mbalimbali za Mfuko kupitia mtandao.
Mratibu wa Mafunzo, Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE), Bw. Albert Rukeisa, akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki w asemina wakifuatilia mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki w asemina wakifuatilia mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki w asemina wakifuatilia mafunzo hayo.
Maafisa wa juu wa WCF, kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, Bi. Laura Kunenge, Bw. Deo Ngowi kutoka Kitengo cha Sheria na Bw. Pascal Richard kutoka Kitengo cha Usajili na Uwasilishaji Michango WCF
Mkurugenzi wa Tiba na Tathmini Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Dkt. Abdulsalaam Omary (kulia) na timu yake ya wataalamu, wakinukuu hoja za washiriki wakati w amaswali na majibu.
Baadhi ya washiriki w asemina wakifuatilia mafunzo hayo.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said.
MKURUGENZI Mtendaji wa Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE), Dkt. Aggrey Mlimuka amewaambia waajiri nchini kuwa kujisajili na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi sio hiari bali ni lazima.
Dkt. Mlimuka ameyasema hayo Alhamisi Novemba 28, 2019 jijini Dar es Salaam wakati akifungua mafunzo ya siku moja yaliyoandaliwa na ATE kwa kushirikiana na WCF na kuwaleta pamoja waajiri kutoka sehemu mbalimbali nchini ili kujifunza kuhusu masuala ya Fidia kwa Wafanyakazi.
“Naomba tuelewane toka mapema, siyo hiari kujiunga na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi hilo ni takwa la kisheria Mfuko huu uko pale kisheria na ni vema likaeleweka mapema.”Alisema Dkt. Mlimuka
Alisema Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) kiko kwa maslahi ya waajiri lakini pia kwa maslahi ya waajiriwa (wafanyakazi) kwani wameajiriwa ili kufanya shughuli mbalimbali na wanaweza kuumia au kupatwa na madhara yoyote wakati wakitekeleza majukumu yao na ndio maana upo Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ambao umeundwa maalum kushughulikia masuala hayo.
“Niwashukuru sana viongozi wa WCF kwa kuja hapa leo kutupatia mafunzo, sisi waajiri tutanufaika vya kutosha na mafunzo haya ambayo yataweza kujibu maswali yaliyo mengi kutokana na changamoto mbalimbali.” Alibainisha Dkt. Mlimuka.
Alisema,hapo zamani malipo ya Fidia kwa Mfanyakazi aliyeumia yalikuwa kidogo sana, na ndio maana Serikali ikaanzisha Mfuko huu ambao kwa kweli umesaidia sana katika kutatua changamoto zilizokuwa zikitukabili kutokana na masuala ya Fidia.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Dkt. Abdulsalaam Omary alisema, Waajiri wanao wajibu wa kuhakikisha usalama wa wafanyakazi wao unapewa umuhimu wa kwanza na ndio maana WCF inatoa elimu mara kwa mara.
“Ifahamike kuwa sisi WCF wajibu wetu wa msingi ni kulipa fidia stahiki na kwa wakati kwa mfanyakazi aliyeumia, kuugua au kufariki wakati akitekeleza wajibu wake wa kazi… kusajili na kupokea michango kutoka kwa waajiri walio katika sekta ya umma na binafsi Tanzania Bara, lakini pia tunalo jukumu la kisheria la kukuza mbinu za kuzuia ajali na vifo kazini kwa kutoa elimu kwa waajiri lakini pia wafanyakazi wenyewe na hiki ndicho tunachokifanya hapa leo.” Alisema Dkt. Omary wakati akiwasilisha mada yake ya namna ya kudai Fidia.
Washiriki hao walipatiwa mafunzo mbalimbali yakiwemo Sheria iliyoanzisha Mfuko, Kujisajili na jinsi ya kuwasilisha michango WCF na namna ya kuwasilisha madai ya Fidia, Mafao yanayotolewa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi na huduma za WCF kupitia Mtandao.
Toa Maoni Yako:
0 comments: