Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida,  Elia Digha, akizungumza juzi katika Harambee ya ujenzi wa Msikiti wa Zaharau uliopo katika Kata ya Ughadi "B" Halmashauri ya wilaya hiyo.
 Msikiti wa Zaharau uliopo katika Kata ya Ughadi "B" Halmashauri ya wilaya hiyo ambao unatakiwa kujengwa.
 Waumini wa dini ya kiislam wakiwa kwenye harambee hiyo.
 Michango ikihesabiwa.
 Katibu wa Msikiti huo Sheikh Ismail Issa, akizungumza.
Waumini wa dini ya kiislam wakiwa kwenye harambee hiyo.

Na Boniphace Jilili Singida. 

MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida,  Elia Digha ameitaka jamii kuondokana na vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyoendelea kujitokeza katika jamii. 

Elia Digha aliyasema hayo juzi wakati akiendesha harambee ya ujenzi wa jengo la Msikiti wa ZAHARAU uliopo katika kata ya Ughadi "B" Halmashauri ya wilaya hiyo ambapo alichangia Mabati 50, na sh. laki 3.

Mwenyekiti huyo alisema kumekuwa na vitendo vya wanaume kuwalawiti watoto, ambapo akasema vitendo hivyo havikubaliki katika jamii, na kuwaomba viongozi wa kidini kusaidiana kukemea jambo hilo huku wakimwomba mwenyezi Mungu kuondoa roho za vitendo hivyo mioyoni mwa watu. 

"Baadhi ya wanaume wamekuwa washenzi hawamuongopi hata Mungu wanawalawiti watoto wadogo, wanabaka watoto jamani wapi tunakoelekea"alisema Digha. 

Hata hivyo aliwasisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi katika kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa, pamoja na kujitokeza kwenye zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kwa wenye sifa za kuandikishwa, ambapo ni wapiga kura wapya, waliopoteza ama kuharibikiwa kadi zao na sifa zingine zilizoaishwa na tume ya uchaguzi. 

Digha alikusanya jumla ya sh. milioni 5 laki 5 na 100,kwenye harambee hiyo, fedha taslimu ikiwa ni sh.milioni 1 laki 8 na elfu 31 Mia moja,huku ahadi ikiwa ni sh. milioni 2 na nusu ambapo aliwataka viongozi wa msiki huo kusimamia na kutumia fedha hizo kwa matumizi yaliyotarajiwa ili kukamilisha jengo hilo na waumini waanze kulitumia kwa shughuli za ibada. 

Aidha Katibu wa Msikiti huo Sheikh Ismail Issa wakati akisoma taarifa ya Msikiti alisema jumla ya sh. Milioni 20 zinahitajika kukamilisha jengo hilo ambapo mpaka sasa zaidi ya sh.milioni 9 zimekwisha tumika.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: