Mratibu wa Mradi wa kupinga vitendo vya mila potofu ya ukeketaji na ukatili wa kijinsia dhidi ya mama na mtoto kutoka Shirika la Save Mother and Children Central Tanzania (SMCCT) Evaline Lyimo (katikati) akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Masinda wakati wa tathmini ya mradi huo wilayani Ikungi mkoani Singida mwishoni mwa wiki. Kulia kwake ni Mwezeshaji wa mradi huo, Aloyce Kalegeya.
Diwani wa Kata ya Makhonga Sombi Majuta akizungumza katika kikao cha kutahmini mradi huo akiwa na wajumbe wa kamati ya ulinzi wa mama na mtoto wa kata hiyo.
Lyimo akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Makhonga wanaounda klabu ya kupinga vitendo vya ukatili.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Lainichungu wakiwasikiliza viongozi wa SMCCT walipokuwa katika tathmini ya mradi huo.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Lainichungu wakiwa katika mkutano wa tathmini.
Wanafunzi wanaounda Klabu ya kupinga ukatili wa Shule ya Msingi ya Lainichungu wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa shirika la SMCCT na walimu wao.
Viongozi wa SMCCT wakiwa na wajumbe wa kamati ya ulinzi wa mama na mtoto wa Kata ya Ihanja wakati wakifanya tathmini ya mradi huo.
Hapa Lyimo akizungumza na wanafunzi wanaounda klabu ya watoto ya kupinga ukatili wa Shule ya Msingi Ihanja.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mapambano wakisubiri kuzungumza na viongozi wa SMCCT.
Mratibu wa Mradi huo kutoka Shirika la SMCCT, Evaline Lyimo akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mapambano. .
Mratibu wa Mradi huo kutoka Shirika la SMCCT, Evaline Lyimo akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mapambano.
Kushoto ni Mwezeshaji wa Shirika hilo, Aloyce Kalegeya
Wanafunzi wa Klabu ya kupinga ukatili katika Shule ya Sekondari ya Masinda wakijaza fomu maalumu ya tathmini ya mradi huo.
Hapa akiongea na wanafunzi wa Shule ya Msingi Iseke wanaounda klabu hiyo.
Hapa akiongea na wanafunzi wa Shule ya Msingi Unyangwe wanaounda klabu hiyo.
Hapa akizungumza na kamati ya ulinzi wa mama na mtoto wa Kata ya Iseke.
Na Dotto Mwaibale, Singida.
KAMPENI ya kutokomeza mila potovu za ukeketaji, mimba za utotoni na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa watoto na wanawake wilayani Ikungi mkoani Singida imeanza kufanikiwa.
Mafanikio hayo yamekuja kufuatia kamati za ulinzi wa mama na mtoto na klabu za kupinga vitendo hivyo zilizoundwa na Shirika la Save Mother and Children for Central Tanzania (SMCCT) kuanza kuibua vitendo hivyo na kufanyiwa kazi.
Akizungumza mwishoni mwa wiki katika kampeni maalumu ya siku sita ya kupinga vitendo hivyo na tathmini ya mradi wa utetezi dhidi ya mila potofu na udhalilishaji wa kijinsia, Mratibu wa mradi huo kutoka Shirika hilo la Save Mother, Evaline Lyimo alisema kampeni hiyo imeanza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Alisema kampeni hiyo ambayo imefadhiliwa na Shirika la Foundation for Civil Society (FCS) inayolenga kutokomeza ukeketaji, ukatili wa kijinsia, mimba na ndoa za utotoni dhidi ya watoto pamoja na udhalilishaji wa kijinsia wilayani Ikungi imeanza kufanikiwa baada ya klabu zilizofunguliwa mashuleni na kamati za kumlinda mama na mtoto kuibua vitendo hivyo na kuanza kufanyiwa kazi.
Alisema katika kampeni hiyo shirika hilo limetembelea kata sita na vijiji 18 pamoja na shule 25 zilizopo wilayani humo pamoja na kutathmini mradi huo ambapo waliwa tembelea wahanga wa matukio ya ukatili kama kukeketwa, kubakwa, kulawitiwa na wale ambao wamerudishwa shuleni baada ya kupatiwa elimu na shirika hilo kwa msaada wa kamati za ulinzi wa mama na mtoto na klabu za wanafunzi katika shule za sekobdari na msingi.
SMCCT ni Shirika lisilo la kiserikali ambalo pia Ni mwanachama wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania( THRDC), ambalo limejikita Katika kupinga matukio ya ukatili kupitia mradi huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments: