Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo akiangalia papai alipokuwa akitembelea mabanda ya maonesho ya maadhimisho ya siku ya chakula duniani ambayo kitaifa yanafanyika Uwanja wa Bombadia mkoani Singida. Mratibu wa maonesho hayo, Sadoti Makwaruzi (katikati) akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Ikungi kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya maonesho hayo
na utoaji elimu wa matumizi ya vyakula vyenye virutubisho.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Kilimo, Revocatus Kasimba (kushoto) akitoa taarifa kuhusu hali ya chakula nchini.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo akizungumza na watafiti wa kilimo kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) alipotembelea banda lao. Kutoka kushoto Mtafiti Msaidizi wa Zao la Maharage Tari Selian Arusha, Mtafiti wa Kilimo kutoka Tari Makao Makuu Dodoma, Mshaghuley Ishika na Demetria Mugunda, Mtafiti wa Zao la Maharage kutoka Tari Selian Arusha, Edith Kadege.
Afisa Kilimo Wizara Kilimo Idara ya Afya ya Mimea ( PITS) Twaha Balali (kushoto).akimuelekeza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi matumizi ya dawa za kuua waharibifu wa mazao.
Mushema Ayubu kutoka Wizara ya Kilimo Dodoma akimuelekeza kuhusu matumizi ya mbegu Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo alipotembelea banda hilo.
Na Dotto Mwaibale, Singida
TAFITI zinazofanywa na wataalamu wa kilimo wametakiwa kuzipeleka kwa wananchi badala ya kubaki nazo ofisini ili zikawasaidie wananchi.
Wito huo umetolewa leo na Mkuu wa wilaya ya Ikungi Edward Mpogolo wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonesho ya maadhimisho ya siku ya chakula kitaifa Mkoani Singida.
Alisema wataalamu hao wanapaswa kutoa semina mbalimbali kwa maafisa ugani huko Wilayani ili na wao wakawasaidie wananchi kupata utaalamu mbalimbali wa masuala ya kilimo.
Mpogolo ameyapongeza mashirika ya Save the Children Tanzania,WFP, na FAO kwa kuendelea kuisaidia Tanzania katika masuala ya kilimo, huku akiweka bayana hali ya upatikanaji wa chakula katika wilaya yake kuwa inachakula cha kutosha,kinachopaswa ni wananchi wake kupatiwa elimu ya lishe bora.
Awali akimkaribisha Mkuu wa wilaya, Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Serikalini Wizara ya Kilimo, Revocatus Kassimba alisema maonesho hayo yanatoa hamasa ya ulaji wa vyakula bora na kuwapa elimu wananchi kuhusu vyakula vyenye virutubisho.
Toa Maoni Yako:
0 comments: