Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa SADC wa Sekta ya TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa wanakutana kwa siku mbili kuanzia leo Septemba 19-20, 2019 jijini Dar es Salaam. Picha zote na Matokeo Chanya+.

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewataka mawaziri wanaoshughulikia tehama, habari, uchukuzi na hali ya hewa kutoka nchi 16 wanachama wa Jumuiya ya maendeleo ya nchi kusini mwa Afrika (SADC) kusimamia maendeleo ya teknolojia.

Hayo ameyasema leo Septemba 19, 2019 wakati akizindua mkutano wa mawaziri hao, ambao ulitanguliwa na majadiliano yaliyowakutanisha makatibu wakuu na viongozi wa juu wanaoshughulikia sekta hizo kutoka nchi wanachama ambao walikaa kwa siku tatu kabla ya baraza la mawaziri lililoanza juzi.

Kati ya maagizo hayo ni pamoja na kushughulikia masuala ya mtandao, mkakati wa posta kuurejesha katika teknolojia ya sasa, kuondoa vikwazo vya kibiashara kati ya nchi na nchi, maendeleo kiteknolojia.

Katika hotuba yake, amesema mkutano huo ni wa kwanza kisekta baada ya mkutano wa awali.

“Ni matarajio yetu kuwa mkutano huu utajadili utekelezaji wa mikakati mbalimbali, programu na miradi kama ilivyoainishwa kwenye mpango mkakati elekezi wa maendeleo ya sadc wa mwaka 2015 mpaka 2030.

“Pamoja na mpango kabambe wa maendeleo ya miundombinu wa mwaka 2019 mpaka 2023 utajadili na kufanya tathmini na kuja na njia mbadala ya utekelezaji uchumi kikanda ili kuharakishwa,” alisema.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhandisi Isack Kamwelwe akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa SADC wa Sekta ya TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa wanakutana kuanzia leo Septemba 19-20, 2019 jijini Dar es Salaam.

Nae Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe amesema mkutano huo umewakutanisha wataalamu wa tehama, hali ya hema, uchukuzi na mawasiliano kutoka nchi wanachama pamoja na wakuu wa taasisi na mashirika pamoja na viongozi waliopo katika sekta binafsi nchi za SADC.

Amesema katika majadiliano wote kwa pamoja wanazo changamoto mbalimbali wanazoshabihiana katika hali ya hewa, miundombinu mbalimbali ambayo inarudisha nyuma nchi kujikomboa kiuchumi na kuwa wana mjadala wa pamoja katika kuzileta nchi kiuchumi kwa manufaa ya wananchi wa ukanda huu.

“Kipindi cha asubuhi tumeshaanza na tumeendelea na mjadala wajumbe walileta hoja mbalimbali kushuhghulikia reli, majanga na hali ya hewa, manufaa ya teknolojia ya habari na mawasiliano katika kuboresha uchumi na maisha ya wana SADC.

“Aidha wataalamu kutoka sekta za kibenki maendeleo ya Afrika na Benki ya Maendeleo ya Afrika Kusini wameelezea uwezo wao katika kusaidia ujenzi na uboreshaji wa miundombinu katika sadc, lakini pia maeneo mengine yaliyoangaziwa ni pamoja na ushirikishwaji wa wanawake na sekta binafsi,” amesema Kamwelwe.
Mkurugenzi wa Miundombinu wa SADC, Mapolao Mokoena amesema mkutano huo utaweza kusaidia uelewa wa watendaji wa Serikali kujua njia ya kupita katika kuifanya jumuiya ifikie malengo yake hasa katika miundombinu.
Mawaziri wa SADC wa Sekta ya TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa wanakutana kwa siku mbili kuanzia leo Septemba 19-20, 2019 jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akiwa na Mkurugenzi wa Miundombinu wa SADC, Mapolao Mokoena (kushoto).
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhandisi Isack Kamwelwe (wa kwanza kushoto) akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (katikati) pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Sekta ya Uchukuzi Bw. Leonard Chamriho.
Mawaziri wa SADC wa Sekta ya TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa wanakutana kwa siku mbili kuanzia leo Septemba 19-20, 2019 jijini Dar es Salaam.

Meza kuu.
Meza kuu wakiendelea na majadiliano.

Mawaziri wa SADC wa Sekta ya TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa wakiuliza maswali wakati wa majadiliano.
Majadiliano yakiendelea...
Mawaziri wa SADC wa Sekta ya TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa wanakutana kwa siku mbili kuanzia leo Septemba 19-20, 2019 jijini Dar es Salaam.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: