RAIS wa zamani wa nchini Zimbabwe, Robart Mugabe amefariki dunia akiwa na miaka 95 huko nchini Singapore alipokuwa akipata matiabu.

Hayati Mugabe aliongoza nchi ya Zimbabwe kuanzia mwaka 1980 hadi 2017 ambapo alipata mrithi wake ambaye ni Rais wa sasa wa nchi hiyo, Emmerson Mnangagwa.

Mugabe alizaliwa Februari 21, 1924 kwenye koloni la Rhodesia.

Rais Mugabe ambaye alionekana akisema maneno mengi ya masihara katika mtandao ya kijamii na yenye ukweli ndani yake kama "SOMETIMES YOU LOOK BACK TO YOUR AT GIRLS YOU SPEND MONEY ON RATHER IT TO YOUR MUM AND REALISE WITCHCRAFT IS REAL".

Pengine unaweza kusema Mugabe ni Rais aliyekuwa na shahada nyingi kuliko walio wengi, Mugabe alikuwa na shahada saba. Digrii yake ya kwanza alipata kutoka chuo kikuu cha Fort Hare, Afrika Kusini na shahada zake nyinginealisoma kupitia mtandao akiwa gerezani.

Hata hivyo Mugabe alipohojiwa na BBC Kuhusu afya yake, alisema," Nimekufa mara nyingi hapo ndipo nimemshinda Yesu Kristo. Yesu alikufa mara moja, na akafufuka mara moja," alisema alipotimiza miaka 88. Ingawa kwa sasa hatuponae tena.

Pia Mugabe wakati wa uhai wake hakuwa mpenzi wa mpira wa miguu ila baadae utu uzima ulipomfikia alikuwa akiangalia mpira wa miguu na kuwa hasa shabiki namba moja wa timu ya Chelsea na Barcelona.

Lakini Mugabe enzi za uhai wake alikuwa mapenzi ya mchezo wa kriketi, akiwa mlezi wa jumuiya ya mchezo wa kriketi nchini Zimbabwe na nyumba na alipokuwa akiishi alikuwa karibu na uga wa michezo huo huko Harare.

Kuhusu familia yake Mugabe alikuwa na watoto watatu na mke wake wa pili, Grace Marufu, aliyekuwa karani wake. Mtoto wao wa tatu alizaliwa 1997 wakati huo yeye akiwa na miaka 73, mwaka mmoja baada ya kufunga ndoa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: