Mkurugenzi Mkuu wa Lodhia Group of Companies, Harminder Bhachu akieleza kuhusu namna Nondo zinavyotengenezwa hatua kwa hatua na hatimaye kupelekwa sokoni kwa kuuzwa,mbele ya Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda waliotembelea kiwanda hicho kwa ajili ya kuangalia ubora wa bidhaa na mazingira ya uzalishaji kwa Tanzania.
Bhachu alisema kampuni hiyo ilianzishwa mwaka 1996 wakiwa wanafanya biashara ya jumla ya kuuza vyuma ambapo mwaka 2004 ndio walianza kuzalisha vyuma katika kiwanda kilichopo mkoani Arusha.“Vilevile tuligeukia bidhaa nyingine ikiwemo mabomba ya maji, Gypsum Board, mapipa ya kuhifadhia maji na bidhaa nyingine za ujenzi kwa kuhakikisha Tanzania inajitosheleza katika vifaa vya ujenzi bila kuagiza nje ya nchi,” alisema Bhachu na kuongeza.
Mkurugeni wa Kampuni ya Lodhia Group of Companies Sailesh Pandit akiwaongoza Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda waliotembelea kiwanda hicho leo kwa ajili ya kuangalia ubora wa bidhaa na mazingira ya uzalishaji kwa Tanzania.
Mkurugenzi Mkuu wa Lodhia Group of Companies, Harminder Bhachu akiwaonesha Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC nondo zikiwa tayari kusafirishwa maeneo mbalimbali kwa matumizi.
Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda wakiangalia namna mabomba ya Platic yanavyotengenezwa ndani ya kiwanda cha Lodhia Group of Companies, hatua kwa hatua na hatimaye tayari kwa matumizi
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Toni Filbert akizungumza mbele ya Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda (hawapo pichani) mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea kiwanda cha Lodhia Group of Companies,kilichopo wilayani humo mkoani Pwani,Mh.Filbert alisema wilaya hiyo pamoja na Mkoa wa Pwani kwa ujumla wanazo fursa nyingi za uwekezaji kutokana na ardhi kubwa yenye rutuba. Vilevile, kuna bidhaa nyingi za kimkakati zinazozalishwa na wazawa.
“Tunaihakikishia serikali kuwa kazi tunaiweza, tutatoa fursa za ajira na kuzifanyia kazi rasilimali tulizonazo kwa ajili ya Tanzania mpya ya viwanda. Tunaomba, kampuni kama hizi za kimkakati zipewe fursa katika kushiriki ujenzi wa miradi mikubwa ikiwemo SGR na miradi mingine ikiwemo madaraja na barabara,” alisema Filbert.
Mkurugeni wa Kampuni ya Lodhia Group of Companies, Sailesh Pandit akisoma hotuba yake fupi mbele ya Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda,ambao wametembelea kiwanda hicho leo kwa ajili ya kuangalia ubora wa bidhaa na mazingira ya uzalishaji kwa Tanzania.
Mkurugeni wa Kampuni ya Lodhia Group of Companies, Sailesh Pandit akizungumza na baadhi ya Waandishi wa habari walioambatana na Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda,ambao wametembelea kiwanda hicho leo kwa ajili ya kuangalia ubora wa bidhaa na mazingira ya uzalishaji kwa Tanzania.
Mkurugenzi wa Mahusiano Bakharesa Group, Hussein Sufian akitoa ufafanuzi wa jambo mbele ya wajumbe wa SADC waliopata fursa ya kutembelea kiwanda hicho cha kusindika matunda cha Bakhresa Group of Companies kilichopo Mwandege Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.Katika ziara hiyo Wajumbe walivutiwa na namna ya kipekee waliyoonesha wafanyakazi wa kiwanda hicho katika usindikaji matunda, mitambo ya kisasa na usafi wa hali ya juu,huku ikionesha pia ni namna gani kampuni hiyo ilivyo tayari kuliteka soko la SADC.
Akielezea uwekezaji huo mkubwa uliogharimu Dola za Kimarekani Milioni 210, Mkurugenzi wa Mahusiano Bakharesa Group, Hussein Sufian alisema kampuni hiyo ina viwanda mbalimbali vipatavyo vinne ambavyo vinasindika bidhaa za chakula.“Soko letu baada ya kujitosheleza ndani tulijipanua katika mataifa mbalimbali ya kiafrika, kwenye muktadha wa SADC tunafikisha bidhaa zetu katika nchi saba ukiondoa Tanzania, ambazo ni DRC, Angola, Comoro, Msumbiji, Malawi, Zimbabwe na Afrika Kuisini.
Mkurugenzi wa Mahusiano Bakharesa Group, Hussein Sufian akitoa ufafanuzi wa jambo mbele ya wajumbe wa SADC waliopata fursa ya kutembelea kiwanda hicho cha kusindika matunda cha Bakharesa Group of Companies kilichopo Mwandege Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.
Mkurugenzi wa Biotan Group Limited,Bahati Mayoma akizungumza mbele ya Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda na baadaye walitembelea kiwanda hicho cha kusindika Korosho kilichopo Mkuranga mkoani Pwani , Wajumbe hao walijionea hatua kwa hatua namna korosho zinavyopokewa kutoka kwa wakulima, zinavyopangwa kwa daraja, zinavyochemshwa kwa kutumia mvuke hadi hatua ya kuzibangua zikiwa tayari kwa kuwekwa kwenye mifuko.
Akizungumzia kuhusu soko,Mayoma alibainisha kuwa wanaliona soko la SADC muhimu kwao kwa kuwa kitu muhimu kinachotakiwa katika kulifikia soko hilo ni kuwa na bidhaa zenye ubora ambazo zinaandaliwa katika mazingira safi na salama kwa kutumia teknolijia za hali ya juu.Alisema kwa mwaka uwezo wao wa kuzalisha ni tani 1500 hadi 2000, lakini wanatarajia baada ya kuliteka soko la SADC ikifika mwaka 2021 uwezo wa uzalishaji utafikia tani 5000 kwa mwaka.
Baadhi akina mama wakibangua korosho ndani ya kiwanda cha BIOTAN,kilichopo Mkuranga mkoani Pwani,Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda na baadaye walitembelea kiwanda hicho cha kusindika Korosho kilichopo Mkuranga mkoani Pwani , Wajumbe hao walijionea hatua kwa hatua namna korosho zinavyopokewa kutoka kwa wakulima, zinavyopangwa kwa daraja, zinavyochemshwa kwa kutumia mvuke hadi hatua ya kuzibangua zikiwa tayari kwa kuwekwa kwenye mifuko. Picha na Michuzi JR.
Na Ripota Wetu.
WAJUMBE wa Mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo kwa Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC) wametapa nafasi ya kutembelea viwanda 21vinavyofanya uzalishaji kwa ajili ya kuangalia ubora wa bidhaa na mazingira ya uzalishaji kwa Tanzania Bara na Zanzibar.
Wakiwa katika viwanda hivyo wajumbe hao wamekiri na kuridhishwa na ambavyo Serikali ya Tanzania namna ilivyodhamiria katika Uwekezaji katika viwanda huku wakieleza wazi Tanzania wanayo nafasi kubwa ya kumiliki soko la Jumuiya hiyo kwani kuna kila.kitu zikiwemo malighafi za uhakika.
Baadhi ya wajumbe wa SADC wameiambia Michuzi TV na Michuzi Blog kuwa Tanzania ipo katika nafasi nzuri ya kulimiliki soko la jumuiya hiyo kwa kuwa kuna nguvu kazi ya kutosha na malighafi za uhakika.
Mjumbe kutoka nchini Afrika Kusini wa Kampuni ya Flexion Renatus Joseph amesema kwamba yeye yupo katika sekta ya viwanda vya chuma jijini Johannesburg, Afrika Kusini na kwamba aliyoyashuhudia katika kiwanda cha Lodha Group of Companies yamenifanya abadili fikra zake kuhusu uwezo wa viwanda kwa nchi ya Tanzania.
Amesema amethibitisha kwa macho yake kuna matumizi makubwa ya teknolojia katika utengenezaji bidhaa za nondo na vifaa vingine vitokanavyo na chuma. "Hakika vikipatikana viwanda vingi vya namna hii SADC tutapiga hatua na tutakuwa na bidhaa zinazoleta ushindani ndani na nje ya Afrika,” amesema.
Wajumbe hao wakiwa kiwandani hapo yameelezwa kiwanda hicho cha chuma kilichopo Mkuranga mkoani Pwani ni miongoni mwa viwanda vilivyoitikia mwito wa Rais Dk. John Magufuli kwa vitendo kuhusu Tanzania ya viwanda.
Akizungumza mbele ya ujumbe wa SADC waliotembelea kiwandani hapo Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Mhandisi Kamara Gombe amesema Tanzania kwa sasa inazalisha tani 200,000 za bidhaa za viwanda huku mahitaji ni tani 300,000.
"Hii maana yake kuna uhaba wa tani laki moja kwenye soko. Hivyo, Kampuni ya Lodhia ni miongoni mwa wadau wa viwanda wanaohakikisha Tanzania inajitegemea katika sekta ya viwanda.Hata hivyo, mbali ya uhitaji huo wa tani laki moja bado kuna tatizo la uhaba wa soko kwa kuwa wanazalisha tani 3000 kwa mwezi
"Lakini uwezo wao ni kuzalisha tani 10,000. Kazi yetu viwanda ni kulinda viwanda vya ndani, tutahakikisha tatizo hili tunalitafutia ufumbuzi ili hizi tani 7,000 zilizobaki ziweze kuzalishwa,” amesema Gombe.
Wakati Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Toni Filbert amesema wilaya hiyo pamoja na Mkoa wa Pwani kwa ujumla wanazo fursa nyingi za uwekezaji kutokana na ardhi kubwa yenye rutuba. Vilevile, kuna bidhaa nyingi za kimkakati zinazozalishwa na wazawa.
Akitoa maelezo kuhusu uwezo wa kiwanda hicho, Mkurugenzi Mkuu wa Lodhia Group of Companies, Harminder Bhachu alisema kampuni hiyo ilianzishwa mwaka 1996 wakiwa wanafanya biashara ya jumla ya kuuza vyuma ambapo mwaka 2004 ndio walianza kuzalisha vyuma katika kiwanda kilichopo mkoani Arusha.
“Vilevile tuligeukia bidhaa nyingine ikiwemo mabomba ya maji, Gypsum Board, mapipa ya kuhifadhia maji na bidhaa nyingine za ujenzi kwa kuhakikisha Tanzania inajitosheleza katika vifaa vya ujenzi bila kuagiza nje ya nchi,” amesema Bhachu na kufafanua wanamshukuru Rais Magufuli kwa kuwahamasisha kuwekeza kwa nguvu na pia amesaidia kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji kwa kila kampuni bila kupendelea.
Hata hivyo katika ziara hiyo, wajumbe wa SADC pia walipata fursa kutembelea kiwanda cha kusindika matunda cha Bakhresa Group of Companies kilichopo Mwandege Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.
Wajumbe walivutiwa na namna ya kipekee waliyoonyesha wafanyakazi wa kiwanda hicho katika usindikaji matunda, mitambo ya kisasa na usafi wa hali ya juu pia ulionyesha ni namna gani kampuni hiyo ilivyo tayari kuliteka soko la SADC.
Akielezea uwekezaji huo mkubwa uliogharimu Dola za Kimarekani Milioni 210, Mkurugenzi wa Mahusiano Bakhresa Group, Hussein Sufian alisema kampuni hiyo ina viwanda mbalimbali vipatavyo vinne ambavyo vinasindika bidhaa za chakula.
“Soko letu baada ya kujitosheleza ndani tulijipanua katika mataifa mbalimbali ya kiafrika, kwenye muktadha wa SADC tunafikisha bidhaa zetu katika nchi saba ukiondoa Tanzania, ambazo ni DRC, Angola, Comoro, Msumbiji, Malawi, Zimbabwe na Afrika Kuisini.
“Katika kuhakikisha tunakuza ajira na kuongeza tija katika uzalishaji, kwa asilimia kubwa malighafi zetu zinatoka Tanzania. Tuna ardhi kubwa inayotuwezesha kukusanya matunda kila kona ya nchi, tunayasindika na kuuza nje ya nchi kwa kiwango cha kutosha. Asilimia 15 ya bidhaa zetu tunazisafirisha nje ya Tanzania hasa hizi nchi za SADC,” ameeleza.
Akizungumza katika kiwanda hiki, Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga amesema watahakikisha wanasimamia haki za msingi za kampuni hiyo kwa sababu imewapa heshima kubwa katika Mkoa wa Pwani kutokana na kupata ajira nyingi za vijana.
Pamoja na mambo mengine wajumbe wametembelea pia kiwanda cha kusindika korosho cha Biotan kilichopo wilayani Mkuranga ambapo Katika kiwanda hiko wajumbe walijionea hatua kwa hatua namna korosho zinavyopokewa kutoka kwa wakulima, zinavyopangwa kwa daraja, zinavyochemshwa kwa kutumia mvuke hadi hatua ya kuzibangua zikiwa tayari kwa kuwekwa kwenye mifuko.
Akizungumza kiwandani hapo Bahati Mayoma ambaye ni Mkurugenzi wa Biotan Group Limited amefafanua kampuni yao kwa kiasi kikubwa kinamilikiwa na raia kutoka Australia, ndiyo maana hata bidhaa zao zinazingatia viwango vya hali ya juu kwa kuwa wanazisafirisha katika nchi za Ulaya.
Ameongeza kuwa wanaliona soko la SADC muhimu kwao kwa kuwa kitu muhimu kinachotakiwa katika kulifikia soko hilo ni kuwa na bidhaa zenye ubora ambazo zinaandaliwa katika mazingira safi na salama kwa kutumia teknolijia za hali ya juu.
“Bidhaa zetu tunazipeleka Denmark, Sweden, Ujerumani, Australia na nchi nyingine nyingi za kiafrika. Lakini kwa sasa soko letu jipya tunaangalia hizi nchi za SADC,” amesema Mayoma.
Amesema kwamba kwa mwaka uwezo wao wa kuzalisha ni tani 1500 hadi 2000, lakini wanatarajia baada ya kuliteka soko la SADC ikifika mwaka 2021 uwezo wa uzalishaji utafikia tani 5000 kwa mwaka.
Kwa kukumbusha tu SADC ni jumuiya ya kimaendeleo ya kiuchumi inayohusisha nchi wanachama 16 ambazo ni Tanzania, Msumbiji, Zambia, Zimbabwe, Malawi, Angola, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Ushelisheli, Comoro, Botswana, Eswatini, Lesotho, Madagascar, Afrika Kusini, Mauritius na Namibia. Kwa mwaka huu mkutano wa wakuu wa nchi wanachama utafanyika Tanzania kuanzia Agosti 17 hadi 18 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Julius Nyerere (JNICC).
Toa Maoni Yako:
0 comments: