Meneja Masoko wa Huduma za Kifedha Vodacom Tanzania Noel Mazoya (kulia) akifafanua jambo wakati akiongea na wanahabari wakati wa maonesho ya viwanda kwa nchi za SADC yanayofanyika jijini Dar es Salaam. Pembeni Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Alex Bitekeye. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Naibu Waziri wa viwanda na Biashara, Injinia Stella Manyanya (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Alex Bitekeye mara baada ya kutembelea banda la Vodacom Tanzania wakati wa maonesho ya wiki ya viwanda vya nchi za SADC.
Naibu Waziri wa viwanda na Biashara, Injinia Stella Manyanya (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Alex Bitekeye.
Naibu Waziri wa viwanda na Biashara, Injinia Stella Manyanya (kulia) akizungumza machache na Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Alex Bitekeye mara baada ya kutembelea banda la Vodacom Tanzania wakati wa maonesho ya wiki ya viwanda vya nchi za SADC.
Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakitoa huduma mara baada ya kutembelea banda la Vodacom Tanzania wakati wa maonesho ya wiki ya viwanda vya nchi za SADC.
---
KAMPUNI ya Simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania imesema kuna maeneo mengi ambayo wao wamekuwa wakitoa huduma kwa nchi za Jumuiya za Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) huku ikieleza kuwa kupitia maonesho haya wamabaini kuna fursa nyingi za wao kuendelea kujitanua na kutoa huduma kwa nchi hizo.

Pia imesema kuna maeneo matatu ambayo Vodacom wanayaangalia katika kuhakikisha nchi za SADC zinapiga hatua kimaendeleo na kwamba uwepo wao kwenye maonesho hayo ni kuendeleza dhana ya kuwahamasisha wananchi wa nchi hizo kuingia kwenye ulimwengu wa kidijitali.

Meneja Masoko wa Huduma za Kifedha wa Vodacom Tanzania Noel Mazoya amefafanua kwamba wapo kwenye maonesho haya ya viwanda kwa nchi za SADC ili kuhakikisha wanatumia nafasi hiyo kuelezea huduma ambazo wanazitoa na zimekuwa mchango mkubwa wa kukuza uchumi wa nchi za jumuiya hiyo.

Pia amesema kuna maeneo matatu ambayo Vodacom Tanzania wamekuwa wakiyafanya katika kutoa huduma na ametaja eneo la kwanza ni huduma za kifedha ambazo wanazifanya kupitia M Pesa kwani imesaidia wananchi wengi ambao hawajafikiwa na huduma za kifedha kufikiwa kupitia M pesa.

“Ripoti ya mwaka 2017 inaonesha kuwa huduma za kifedha zimefikia wananchi kwa asilimia 65 nchini Tanzania.Ukweli ni kwamba Vodacom Tanzania tumetoa mchango mkubwa katika eneo hilo kutokana na uwepo wa huduma ya M-pesa kupitia huduma jumuishi za kifedha,”amesema Mazoya.

Amefafanua eneo lingine muhimu ambalo wamejikita kuwa ni huduma ya intaneti kwenye nchi za SADC kwa kuhakikisha wananchi wanapata intaneti ya uhakika na ya urahisi na kwa kufanya hivyo inawasaidia kuwa sehemu ya kufanya biashara ya kununua bidhaa na huduma kupitia njia ya mtandao.

“Katika eneo hilo tumejipanga kuhakikisha nchi za SADC zinashirki kwenye uchumi wa kidunia kupitia ulimwengu wa intanet. Kwa mfano Vodacom Tanzania tunayo huduma ya kumuwezesha  Mtanzania kununua bidhaa kwa njia ya mtandao kupitia ushirikiano wetu na Master Card,”amesema.

Wakati eneo la tatu ni la 5G na kwamba mkakati uliopo kwa sasa ni kutoka kwenye kasi ya 4G na kwenda kasi ya 5G na kufafanua nchi ya Lesotho tayari wapo kwenye kasi ya 5G na hiyo maana yake ni kuwafanya wananchi ajue na kuamini kwamba mtandao ni sehemu ya maisha yao ya kila siku.

Kuhusu maonesho hayo amesema kuwa kikubwa ambacho wamekiona ni uwepo wa fursa nyingi na hasa za ujasiriamali na kufafanua kuwa wao wameona fursa katika kuendelea kupata kampuni nyingi zaidi ambazo wanaweza kuzihudumia nchini.

“Kuna fursa ambazo tumeziona na ukweli ni nyingi na tumejifunza mambo mengi kutoka kwa wenzetu kwa mfano Lesotho wao wapo kwenye 5G na hivyo kuna mambo ya kujifunza kutoka kwao lakini wakati huo huo nchi nyingi za SADC nazo zinajifunza kutoka Tanzania kwani nyingi hazina huduma za kifedha kwa njia ya mtandao wa simu za mkononi ambazo sisi na Kenya tumefanikiwa sana,”amesema Mazoya.


Hata hivvyo amesema kuwa Vodacom wanaiona jumuiya ya nchi za SADC ni eneo muhimu kwao na wataitumia jumuiya hiyo kutoa huduma kwa kampuni mbalimbali za ndani na nje ya na kampuni yao ipo kwa ajili hiyo kuhakikisha nchi hizo zinasonga mbele kimaendeleo. “Kwetu tumeendelea kupata fursa nzuri zaidi ya kutangaza huduma tunazitoa,”amesema Mazoya
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: