Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Petroli Tanzania(TPDC) James Mataragio wakati anazungumza kwenye mjadala katika wiki ya Viwanda kwa nchi za SADC ambao mada yake ilijikita kuzungumzia mafuta na ujenzi wa miundombinu katika kuondoa umasikini. 
Washiriki wakiendelea kufuatilia mjadala kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TPDC James Mataragio wakati anatoa uzoefuwashirika hilo katika eneo la mafuta ,gesi na ujenzi wa miundombinu
Maelezo. 
Mmoja ya washiriki akiuliza swali.
Muongoza mada akimuuliza wali Mkurugenzi Mkuu wa TPDC James Mataragio.
Mkurugenzi Mkuu wa TPDC James Mataragio akiongea na wanahabari.

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Shirika la Maendeleo la Petroli Tanzania (TPDC) limezihakikisha nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika(SADC) kuwa wana gesi ya kutosha na wanajivunia kuwa na uzoefu wa miaka 50 katika ujenzi wa miundombinu ya gesi na mafuta.

Pia limesema kwa sasa mahitaji ya gesi yanaongezeka na tayari wameanza kufanya mazungumzo na nchi tano za Kenya, Zambia, Uganda , Malawi na DRC ili wapelekewe gesi kwenye nchi zao.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa TPDC James Mataragio wakati anazungumza na waandishi waliokuwa kwenye mjadala ambao mada yake ilijikita kuzungumzia mafuta na ujenzi wa miundombinu katika kuondoa umasikini.

Hivyo wametumia nafasi hiyo kueleza kuwa mahitaji ya gesi kwa nchi mbalimbali za SADC ni makubwa na ndio maana kuna nchi wanaendelea kuzungumza nazo ili kuhakikisha nishati ya gesi inawafikia.

“Kuhusu nafasi ya soko ya gesi, mahitaji ni makubwa na yanaongezeka kila siku .Nchi za Kenya, Zambia, Uganda , Malawi na DRC wameomba kusambaziwa gesi.

“Hivyo kuna uwezekano wa kujenga bomba la gesi kutoka Dar es Salaam kwenda Mombasa, kujenga bomba la gesi kutoka Tanga kwenda Uganda na tayari kuna uwezekano wa kutumia mkuza wa kupitisha mafuta mazito kwenda Ndola Zambia ambalo litatumika kupitisha gesi,”amesema Mataragio.

Alipoulizwa kuhusu nafasi ya TPDC ,Mataragio amejibu wao wamekuwa na uzoefu mkuwa katika eneo la mafuta na gesi na wamekuwa wakifanya tafiti nyingi katika eneo hilo ikiwemo kugundua mafuta na gesi.

“Tanzania tunao uzoefu kwa miaka 50 katika ujenzi wa miundombinu na hasa kwenye gesi na mafuta. Kuna mabonda kama nne ambayo tumewahi kujenga.Tumejenga bomba kutoka Tanzania kwenda Zambia ambalo linasafarisha mafuta mazito.

“Tumejenga bomba kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam kwa ajili kusafirisha gesi, bomba la Msimbati hadi Mtwara na bomba la kutoka Songo songo kwenda Dar es Salaam,”amesema.

Hivyo amesema wao wametumia majadiliano hayo kuelezea uzoefu wao katika kujenga miundombinu hiyo pamoja na kuisimamia na kwa sasa kuna ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda kuja Tanzania.

Pia amesema ujumbe ambao washiriki wa majadiliano hayo wameupata kutoka kwao ni kwamba wataondoka na ujumbe Tanzania imejiimarisha kwenye miundombinu ya gesi na mafuta pamoja na uwekezaji wa uhakika katika sekta hiyo.

Kuhusu hali ya mafuta nchini amesema ni nzuri na kuna tafiti zinaendelea kwenye maeneo mbalimbali nchini ambako kunaonekana kuna dalili za uwepo wa mafuta.Kuhusu mahitaji ya gesi nchini amesema ni kama futi za ujazo milioni 200 na sehemu kubwa ya gesi inatumika kuzalisha umeme na mchukuaji mkubwa ni TANESCO kwa zaidi ya asilimia 50.

“Pia matumizi ya gesi yanaongezeka kila siku na ndio maana kwa sasa tunaendelea kufanya utafiti wa gesi na mafuta endelevu ili kuhakikisha tunakuwa na nishati hiyo kwa miaka mingi ijayo na kazi hiyo tunaifanya sisi wenyewe,”amesema.

Pia amesema wanaendelea kujenga miundombinu ili kusambaza gesi majumbani na viwandani huku akisisitiza TPDC wamejipanga kuhakikisha na gesi inakuwa endelevu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: