Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Hatimaye Kiswahili kuwa lugha ya Nne rasmi itakayotumika katika mikutano na machapisho mbali mbali ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Akitangaza katika Mkutano wa 39 wa wakuu wa nchi na serikali za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Mwenyekiti wa SADC Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli unaofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania amesema amefurahishwa na jinsi wakuu wenzake wa nchi kuweza kupitisha azimio la kukubali kiswahili kuwa lugha rasmi.

"Kuingiza Kiswahili katika SADC tumefuta machozi ya Hayati Baba Wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye alijitahidi kupigania uhuru wa nchi nyingi za kusini mwa Afrika," amesema Rais Dkt. Magufuli.

Amesema kuwa Kuingiza Kiswahili kutaweza kukuza Ushirikiano na Mshikamano wa nchi za kusini zote za Kusini mwa Afrika.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: