Makamu wa Pili wa Rais, Serikali ya Mainduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi(wapili kushoto), akimkabidhi tuzo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Abraham Siyovelwa wakati wa hafla ya kufunga rasmi maonesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, Julai 11, 2019. WCF imetwaa tuzo ya mshindi wa pili kundi la Taasisi za Hifadho ya Jamii na Bima. Maonesho hayo yatafikia kilele Julai 13, 2019. 

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa, (wapili kushoto), akimpongeza Bw. Siyovelwa kwa tuzo hiyo.
Balozi Seif Ali Iddi akihutubia katika hafla hiyo.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa, akitoa hotuba yake.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano WCF, Bi. Laura Kunenge (mwenye nguo nyeupe), akifuatilia utoaji wa tuzo hizo
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Abraham Siyovelwa (mwenye tai nyekundu), akiwa kwenye hafla hiyo kabla ya kuitwa kupokea tuzo hiyo.
Bw. Siyovelwa akiwa na timu iliyokuwa ikitoa huduma kwenye banda la WCF ,mara baada ya kupokea tuzo hiyo.
Afisa Uhusiano WCF, Bi. Sarah (kushoto), akimpatia maelezo mwananchi huyu aliyetembelea banda la WCF Julai 11, 2019.

Na K-VIS BLOG/Khalfan Said.


MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umetwaa tuzo ya mshindi wa pili kundi la Sekta ya Hifadhi ya Jamii pamoja na Sekta ya Bima kwa kuwa banda lililotoa huduma bora kwenye maonesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam 2019 katika kundi hilo.

Makamu wa Pili wa Rais, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi ndiye aliyemkabidhi tuzo hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Abraham Siyovelwa wakati wa hafla ya ufungaji rasmi wa maonesho hayo kwenye ukumbi wa Rashid Mfaume Kawawa (Ceremonial dome), uwanja wa Maonesho wa Mwalimu J.K Nyerere, maarufu Sabasaba, barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam Julai 11, 2019.

Ufungaji huo ni sehemu tu ya taratibu lakini maonesho yataendelea hadi Julai 13, 2019, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uendelezaji Biashara (TanTrade),ambao ndio waandaaji wa maonesho hayo, Bw. Edwin Mutageruka alisema.

Akizungumzia ushidi huo Bw. Siyovelwa alisema, “Tunafuraha kubwa kama Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, huu ni mwaka wa pili tunapata tuzo na mwaka huu tumepanda zaidi mwaka jana tulishinda kwenye Sekta ya Hifadhi ya Jamii lakini mwaka huu tumekuwa washindi wa pili kwenye Sekta ya Hifadhi ya Jamii pamoja na Bima.” Alifafanua Bw. Siyovelwa ambaye pia ni Mkuu wa Sheria wa Mfuko huo.

Akizungumzia huduma walizokuwa wakitoa kwenye banda la WCF katika maonesho hayo yaliyoshirikisha mataifa zaidi ya 35 kutoka sehemu mbalimbali duniani, Bw. Siyovelwa alifafanua “Pamoja na kutoa huduma nyingine zote lakini tuliona lengo letu liwe kutoa elimu zaidi kwa wafanyakazi na waajiri ya namna ya kudai fidia pale wanapopatwa na matatizo kwa sababu tumeona ni changamoto kubwa ambayo inatukabili.” Alisema.

Aidha alibainisha kuwa WCF imefanya maendeleo makubwa sana katika utoaji wa huduma kwa kupitia TEHAMA, “tumetumia fursa ya maonesho haya kutoa elimu ya huduma zetu mpya ambazo zimejikita katika utoaji wa huduma kupitia TEHAMA, Waajiri hawana haja ya kufika ofisi zetu, wanaweza kupata huduma zote kupitia mtandao.” Alifafanua.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: