Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akimpigia simu mkuu wa polisi wilaya ya Iringa (OCD) kuhakikisha anamkamata popote alipo Ayubu Mwenda ambaye anasababisha mgogoro wa shamba la familia ya mzee Mwenda
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akitoa maelezo kwa familia ya marehemu mzee Mwenda katika kata ya Nduli mkoani Iringa.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amemuagiza mkuu wa polisi wilaya ya Iringa (OCD) kuhakikisha anamkamata popote alipo Ayubu Mwenda kwa kuika makubaliano ya kuumaliza mgogoro huo.
NA FREDY MGUNDA, IRINGA.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amemuagiza mkuu wa polisi wilaya ya Iringa (OCD) kuhakikisha anamkamata popote alipo Ayubu Mwenda ambaye anasababisha mgogoro wa familia ya Mwenda kwa kumkimbia mkuu wa wilaya na kamati yake walipokifika kusuhisha mgogoro huo.
Akizungumza kwenye shamba la familia mzee Mwenda Kasesela alisema kuwa Ayubu Mwenda ameleta dharau kwa kukimbia katika eneo usika la kutatua mgogoro ambao ameusababisha kwa makusudi kwa kutaka kuwadhurumu wanafamilia wenzake.
“Haiwezekani mtu aseme mara yupo mahakamani mara yupo msibani mara anazima simu huu ni utovu wa nidhamu kwa kuwa jana nilikaa nao na tukaongea nao vizuri na yeye akiwepo nay eye ndio chanzo cha mgogoro huo kwanini leo hayupo hapa” alisema Kasesela
Kasesela alisema kuwa familia hiyo inagombea hekali mia moja na hasini na tisa (159) ambazo waliachiwa na marehemu mzee wao mzee Mwenda na kusema kuwa Ayubu ambaye ndiye kaka yao mkubwa amekuwa kisababishi cha mgogoro huo.
Aidha Kasesela alimtaka afisa mtendaji na afisa tarafa kuhakikisha shamba hilo linagawawiwa kwa wake wote sita wa mzee Mwenda ili kuondo na kumaliza mgogoro huo kwa kugawa kwa usawa na haki ili kila mmoja apate haki yake.
“Mzee Mwenda alikuwa na wake sita hivyo shamba hilo litagawiwa kwa kufuata familia za akina mama wote kwa haki ili kumaliza hili tatizo na hakuna mtu mwingine ataleta mgogoro kwa kuwa nitalipeleka shauri hili mahakamani kuweka zuio la kuanzisha kesi yeyoyte ile katika shamba hilo” alisema Kasesela
Kwa upande wake msimamizi wa mirathi hiyo Sadiki Abdalah Mwenda alimshukuru mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela kwa kuasidia kutatua mgogoro huo ambao umedumu kwa miaka mingi bila kupata ufumbuzi wa mgogoro huo.
Naye askari mstaafu Hawa Mwenda ambaye ni mwanafamilia alimshukuru mkuu wa wilaya na kumuomba awafikishie salaam kwa Rais Dr John Pombe Magufuli kwa kuongoza vizuri na kufanikisha wananchi wanyonge wafikiwe kirahisi na kutatuliwa matatizo yao.
Toa Maoni Yako:
0 comments: