Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni wake Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta katika uwanja wa ndege wa Chato mara baada ya kumaliza ziara yake binafsi ya siku mbili Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza mgeni wake Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta wakati wakipita kwenye Gadi ya Heshima iliyoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ katika uwanja wa Ndege wa Chato mkoani Geita.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta wakati wakisikiliza nyimbo iliyokuwa ikiimbwa na wanakwaya wa Mwagazege ya Chato kabla ya Rais Kenyatta kuondoka na kurejea nchini Kenya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mara baada ya mazungumzo yake na mgeni wake Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta Chato mkoani Geita.
Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta akimsalimia Mama mzazi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Bibi Suzana Magufuli ambaye anapatiwa matibabu kijijini kwake Mlimani Chato mkoani Geita kabla ya kuondoka kurejea Kenya mara baada ya kumaliza ziara yake binafsi ya siku mbili.
 Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta akizungumza na wanahabari mara baada ya mazungumzo yake na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta akiweka shada la maua katika moja ya makaburi ya Familia ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli yaliyopo katika kijiji cha Mlimani Chato wakati akiwa katika ziara yake binafsi ya siku mbili.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na mgeni wake Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta kabla ya kuanza mazungumzo yao Chato mkoani Geita.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta mara baada ya mazungumzo yao Chato mkoani Geita.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta  ambaye aliambatana na ujumbe wake kutoka Kenya katika ziara yake binafsi ya siku mbili katika kijiji cha Mlimani Chato Mkoani Geita.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na mgeni wake Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta kabla ya kuondoka katika kijiji cha Mlimani Chato na kurejea nchini kwake Kenya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpungia mkono mgeni wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakati akipanda ndege kurejea nchini Kenya. PICHA NA IKULU

Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Uhuru Muigai Kenyatta tarehe 06 Julai, 2019 amerejea nchini Kenya baada ya kumaliza ziara yake binafsi ya siku 2 aliyomtembelea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika Wilaya ya Chato Mkoani Geita.

Kabla ya kuruka katika uwanja wa ndege wa Chato, Mhe. Rais Kenyatta amefanya mazungumzo ya faragha na mwenyeji wake, Mhe. Rais Magufuli katika Kijiji cha Mlimani na baada ya mazungumzo hayo viongozi hao wamezungumza na waandishi wa habari.

Viongozi hao wamesema mazungumzo yao yalijikita katika kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano wa Tanzania na Kenya hususani katika masuala ya kiuchumi ambapo wametaka biashara baina ya nchi hizo ikuzwe zaidi pamoja na kujenga uwiano wa kibiashara wenye maslahi kwa pande zote.

Mhe. Rais Magufuli amesema kwa kuzingatia kuwa Kenya imefanya uwekezaji mkubwa zaidi nchini Tanzania ikilinganishwa na uwekezaji wa Tanzania nchini Kenya, wamekubaliana kuwa kampuni za Kenya zijielekeza kuongeza thamani ya bidhaa kwa kuanzisha viwanda vitakavyosindika mazao na kuchakata bidhaa mbalimbali hapahapa Tanzania badala ya kusafirisha malighafi kwenda Kenya.

Ameongeza kuwa wamekubaliana kuwa Kenya itanunua gesi ya Tanzania badala ya kuagiza kutoka nje ya Bara la Afrika kwa kuwa Tanzania imejaaliwa gesi nyingi, na wamewaagiza Mawaziri wa Tanzania na Kenya kukutana na kujadili namna Kenya itavyonunua gesi hiyo.

Kuhusu ziwa Victoria ambalo kwa asilimia 51 lipo Tanzania na kwa asilimia 5 lipo Kenya, Mhe. Rais Magufuli amesema wamekubaliana kuwa Mawaziri wa nchi hizo wahakikishe meli za Tanzania na Kenya zinaimarishwa na kuondoa vikwazo vinavyokwamisha meli hizo kufanya kazi ya kukuza biashara katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda ambazo zinazunguka ziwa hilo.

Kwa upande wake, Mhe. Rais Uhuru Kenyatta amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa mapokezi mazuri aliyoyapata hapa Chato, na kwa upendo mkubwa uliooneshwa na wananchi wa Chato kwake na ujumbe wake, na ameeleza kuwa huo ni uthibitisho wa uhusiano mzuri, undugu na urafiki wa karibu wa Wakenya na Watanzania.

Amesema pamoja na kuimarisha zaidi uhusiano wa Tanzania na Kenya uliojengwa na Waasisi wa Mataifa Hayo
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: