Rais Mstaafu wa Awamu na Nne, Mhe. Jakaya Kikwete akipata maelezo mara aada ya kutembelea banda la Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) lililopo katika maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba.
Rais Mstaafu wa Awamu na Nne, Mhe. Jakaya Kikwete akipata maelezo juu ya gari linalotumia mfumo wa gesi.
Rais Mstaafu wa Awamu na Nne, Mhe. Jakaya Kikwete ameliasa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Kikwete ameyasema hayo alipotembelea viwanja vya Maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba.
“Ongezeni kasi ya utekelezaji wa miradi mnayoianzisha ili kuleta tija kwa Taifa na mpunguze michakato” alisema Rais Kikwete. Rais huyo Mstaafu alionyesha kuvutiwa na maelezo mazuri na yenye ueledi yaliyotolewa na watumishi wa TPDC waliokuwa wakitoa huduma bandani hapo.
Aidha Kikwete alitoa changamoto kwa TPDC kuibua miradi mipya yenye tija kwa Taifa na kueleza kwamba miradi mingi iliyopo ni ambayo imekuwepo kwa muda mrefu na ni muda muafaka kwa TPDC kubadilika.
Haya yanakuja ikiwa pia Sheria ya Petroli ya 2015 inaitambua TPDC kama Kampuni ya Taifa ya Mafuta na kuipa mamlaka ya kujiendesha kibiashara na kuwa na haki ya kipekee katika utekelezaji wa miradi ya utafiti, uendelezaji na usambazaji wa gesi asilia.
Akiongea na muandishi wa habari hii, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Mhandisi Kapuulya Musomba alisema katika kuhakikisha utekelezaji wa miradi unafanyika kwa kasi Shirika limejipanga kushirikiana na sekta binafsi katika miradi mbalimbali kama ile ya kusambza gesi majumbani na ya kujenga vituo vya kujazia gesi kwenye magari.
Mhandisi Musomba pia ameeleza uwepo wa kampuni Tanzu mbili za TPDC ambazo zinatekeleza majukumu maalumu kwa niaba ya Shirika Mama.
“GASCO ni moja ya kampuni tanzu ya TPDC ambayo inasimamia miundombinu ya gesi asilia ambayo ni mitambo ya kuchakata pamoja na bomba la kusafirisha gesi asilia na nyingine ni Tanoil Investment Ltd ambayo inajishughulisha na biashara za mafuta” anafafanua zaidi Mhandisi Musomba.
Toa Maoni Yako:
0 comments: