Watu saba wakiwemo wafanyakazi watano wa kampuni ya Azam Media wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori leo asubuhi Jumatatu Julai 8, 2019 katika eneo la Malendi wilayani Iramba mkoani Singida.
Inaelezwa kuwa walikuwa wakieleleka wilayani Chato Mkoa wa Geita katika uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa ya Chato-Burigi unaofanyika kesho Jumanne Julai 9, 2019 na Rais wa Tanzania, John Magufuli.
Taarifa kutoka katika kampuni hiyo zinaeleza kuwa wafanyakazi hao walikuwa katika gari aina ya Coaster na kwamba madereva wawili wa magari hayo nao wamefariki dunia.
Waliofariki dunia watano ni wafanyakazi wa Azam TV na madereva wawili wa gari ya kukodi ambao majina yao bado hayajafahamika.
Wafanyakazi wa Azam Tv waliofariki dunia ni:
Said Haji - Camera man
Charles Wandwi -Camera man
Salim Mhando - Switcher
Florance Ndibalema- Sound
Sylvanus Kasongo - Engineer
Majeruhi
Mohamed Mwinshehe
Mohamed Mainde
Artus Massawe
Mganga mfawidhi wa hospitali ya Igunga Merichad Magongo amethibitisha kupokea majeruhi watatu katika hospitali ya Igunga.
Toa Maoni Yako:
0 comments: