Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoka kukagua eneo la bonde katika mto Rufiji mara baada ya kuweka jiwe la msingi la mradi huo wa umeme.
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG, Rufiji.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli amewaagiza wakala wa barabara nchini (TANROAD) ianze mara moja kujenga barabara kwa kiwango cha lami kuanzia eneo la Fuga ili kuchochea utalii katika Hifadhi hiyo.
Ametoa agizo hilo leo mchana wakati akizungumza na wananchi na viongozi walioshiriki mkutano wa uwekaji wa jiwe la msingi wa Mradi wa kufua Umeme wa maji wa Rufiji ambao utazalisha umeme wa Megawati 22,115.
Amesema fedha na dhahabu zilizorudishwa baada ya kuibiwa hapa nchini na kupatikana nchini Kenya zikatumike kujenga barabara ya lami kutoka lilipo pori la Selous hadi eneo la Fuga inakopita treni ya umeme ya Standard Gauge.
“Juzi nimepokea dhahabu zilizorudishwa kutoka Kenya nimepiga hesabu vizuri ni kama tsh bilioni nne au tano na fedha taslimu kama milioni 500, nataka hizo fedha zianze kutengeneza barabara ya lami kutoka hapa hadi eneo la Fuga ambazo ni kilometa 60 ili watu wakitoka Dar es Salaam kwa treni wakishuka pale Fuga wanatumia barabara hadi hapa kuja kutalii,” amesema.
Aidha ameagiza pia bwawa litakalojengwa kwa ajili ya mradi wa kuzalisha umeme lipewe jina la Mwalimu Nyerere kwani hayo yalikuwa mawazo yake na kufanya hivyo ni kumuenzi.
Toa Maoni Yako:
0 comments: