KATIBU mkuu wa chama cha mapinduzi (CCM) Dkt Bashiru Ally akihutumia wananchi wa monduli wakati wa sherehe za rika zilizofanyika wilayani humo katika kijiji cha mti mmoja
Vijana wa rika la Ooltwati (Nyangulo) wakiwa katika picha ya pamoja wakimsikiliza mgeni Rasmi wa sherehe za Rika ambaye alikuwa KATIBU mkuu wa chama cha mapinduzi (CCM) Dkt Bashiru Ally kwa makini
Vijana wa jamii ya kimasai wa rika la Ooltwati(nyangulo)wakiwa wanaimba na kucheza ngoma zao za asili mbele ya mgeni rasmi.
Katibu mkuu wa chama cha mapinduzi (CCM) Dkt Bashiru Allyakiwa anamuelekeza jambo moja ya viongozi wa rika waliouthuria katika sherehe za kimila za jamiiya kimasai zijulikanazo kwa jina la Ooltwati zilizofanyika katika kijiji cha mti mmoja mmmoja kilichopo kata ya Sepate wilayani Monduli,mkoani Arusha.
Na Woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha.
KATIBU mkuu wa chama cha mapinduzi (CCM) Dkt Bashiru Ally ameitaka jamii ya kimasai kulinda na kudumisha mila zilizotangulia rika zingine.
Dkt Bashiru aliyasema hayo wakati wa sherehe za kimila za jamiiya kimasai zijulikanazo kwa jina la Ooltwati zilizofanyika katika kijiji cha mti mmoja mmmoja kilichopo kata ya Sepate ambapo alisema kuwa mila hizo ninzuri zinaandaa vijana katika nizamu ,heshima huku akiwataka vijana hao wa rika la nyangulo lina kazi kubwa ya kulinda uhuru wa nchi yetu.
Alichukuwa muda huo kuwapongeza viongozi wajamii ya kimasai kwa kurekebisha mila zote mbaya ambazo zilikuwa zinaenda kinyume na tamaduni za mtanzania pamoja na kurekebisha mila zote zilizopitwa na wakati.
"napenda kuwasisitiza nizamu ni jambo linalopaswa kuenziwa na kufuatwa kama mlivyofundishwa na wazee wa marika makubwa waliowatangulia ,pia swala la ulinzi ni muhimu na lazima nanivyema tuheshimu rasilimali za watu wote na labda nisisitize naniwaambie bado tunakazi sana katika swala la aridhi na hii nivita kubwa ambayo tunayo na nilazima tuwe na mipango mikubwa mizuri yakuitumia ili tuweze kuilinda aridhi yetu"alisema Dkt Bashiru
Akiongea katika mkutano huo mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alisema kuwa wao kama viongozi wa serikali walishatatua kero mbalimbali ambazo zilikuwa zikiwakabili wananchi wa wilaya ya Monduli hususa ni ya ardhi na wataendelea kutatua migogoro yote ambayo itajitokeza kwa wananchi hao .
Alibainisha kuwa katika kutetea maslahi ya jamii ya wafugaji ,wao kama serikali pia wanaweka ulinzi katika maeneo ya malisho ya mifugo ili yasiporwe au yasivamiwe.
kwa upande wake mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Amina Mollel aliwataka jamii hio ya kimasai kuendelea kupiga vita swala la ukeketaji wa mabinti pamoja na ndoa za utotoni kwani maswala hayo yote ni mabaya na ukiukaji wa sheria za nchi,alitumia muda huo kuwaasa wananchi hao kuwapeleka watoto wao shule ili waweze kujisaidia hapo baada na kuwa viongozi wasomi wa hapo baadae.
Toa Maoni Yako:
0 comments: