Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko huo, Dkt. Abdulsalaam Omary(kulia), akikabidhi sehemu ya vifaa hivyo kwaMkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu MOI, Dkt. Respisious Binifacewakati wa hafla hiyo Juni 19, 2019.
Dkt. Omary (kulia) na Dkt. Boniface wakiwa wamesimama mbele ya sehemu ya vifaa hivyo.
Dkt. Omary akitoa somo kuhusu majukumu ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), kwa baadhi ya watumishi wa MOI ikiwa ni sehemu ya Wiki ya Uytumishi wa Umma Juni 19, 2019.
Meneja wa Jengo la Upasuaji la Taasisi ya Tiba ya Mifupa Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu MOI, Bi, Elizabeth Mbaga, (kushoto), akizungumza jambo baada ya Dkt. Omary kumaliza kutoa elimu kuhusu Mfuko 
Baadhi ya watumishi wa MOI na wa WCF wakisikiliza maelezo ya Dkt. Omary.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa WCF, Bw. Sebera Fulgence, (wapili kulia), akizunhgumza jambo na mmoja wa wafanyakazi wa MOI.
Meneja wa Jengo la Upasuaji la Taasisi ya Tiba ya Mifupa Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu MOI, Bi, Elizabeth Mbaga, (kushoto), akipokea moja ya vifaa kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Uhusiano na Elimu kwa Umma, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bi. Laura Kunenge.
Mfanyakazi wa WCF akiwa amebeba baadhi ya vifaa vilivyotolewa na Mfuko kama msada kwa taasisi ya MOI.
Baadhi ya wafanyakazi wa WCF wkaiwa kwenye mazungumzo na viongozi wa MOI.
Bi. Laura Kunenga akibadilishana mawazo na wafanyakazi wa jingo la upasuaji la MOI, kutoka kushoto, Bi. Elizabeth ambaye ndiye Meneja wa jingo hilo, Bw.Fidelis, na Mkuu wa Kitengo cha Kukinga na Kudhibiti Maambukizi cha taasisi hiyo, Sister Zaituni Bembe.
Picha ya pamoja baadhi ya wafanyakazi wa WCF waliotembelea MOI katika Wiki ya Utumishi wa Umma, ambapo pamoja na mambo mengine walifanya usafi na kutoa misaada kwa taasisi na wagonjwa.


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said


KWA mujibu wa kalenda ya Umoja wa Afrika (AU), inazitaka nchi wanachama wa umoja huo kushiriki shughuli mbalimbali zinazohusu Utumishi wa Umma kila mwaka.

Hapa nchini mwaka huu Wiki ya utumishi wa umma imeanza Juni 16 na itakamilika Juni 22, 2019.

Leo hii Juni 19, 2019 katika kutimiza wajibu huo, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi umeshiriki shughuli za kujitolea katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI), jijini Dar es Salaam kwa kufanya usafi wa mazingira kuzunguka majengo ya taasisi hiyo, kutoa misaada ya vifaa kwa matumizi ya taasisi na mahitaji ya wagonjwa wanaopatiwa tiba kwenye taasisi hiyo.

Kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko huo, Dkt. Abdulsalaam Omary aliongoza timu ya watumishi wa WCF katika zoezi hilo ambapo pamoja na kufanya shughuli hizo, Dkt. Omary alitumia fursa hiyo kutoa elimu kwa baadhi ya watumishi wa taasisi hiyo ambayo ni mdau mkubwa wa Mfuko.

“MOI ni wadau wetu muhimu, wamekuwa wakitoa huduma mbalimbali kwa wafanyakazi ambao wanapata ajali au magonjwa yatokanayo na kazi, kwa hivyo leo tukiwa kwenye wiki ya utumishi wa umma tumeona bora na sisi watumishi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi tuende katika jamii na kusaidia kwa kadri itakavyowezekana na ndio maana tuko hapa.” Alisema Dkt. Omary.

Alisema Mfuko umetoa vitu mbalimbali vikiwemo vile vya kuhifadhia vifaa vyenye ncha kali kuweka sindano zilizotumika na lengo ni kuweza kuwakinga wafanyakazi wakiwemo wauguzi na madaktariili wasiweze kupata ajali zinazoweza kutokea kutokana na kazi wanazofanya, lakini pia vifaa vya usafi kwa ajili ya wagonjwa hususan watoto waliolazwa hapa wakipatiwa matibabu.

“Pia tulitoa elimu kidogo kwa baadhi ya watumishi wa hapa ili waweze kuelewa shughuli ambazo Mfuko wa Fidia unafanya.” Alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu MOI, Dkt. Respisious Biniface, aliushukuru Mfuko kwa kufika kwenye taasisi yake na kushiriki katika wiki hii ya utumishi wa umma kwa kuwapelekea misaada ikiwa ni pamoja na kufanya usafi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: