Mbunge wa Geita Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akielekea sehemu ya kuzungumzia mara baada ya Mwenge wa Uhuru kuwasili katika eneo la Kalangalala katika Halmashauri ya Geita.
Abiel Damas akisoma taarifa ya kukamilika kwa barabara itakayotumika kwa ajili ya magari yatakayokuwa yamebeba vitu vizito kuelekea migodini kabla ya Mwenge kuzindua barabara hiyo mjini Geita.
Mbunge wa Geita Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ( wa pili kulia) akiwa na baadhi ya viongozi wa Halmashauri ya Geita mjini kabla ya kupokea Mwenge wa Uhuru katika eneo la Kalangalala.
Mbunge wa Geita Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akisalimiana na mmoja wa Wakimbiza Mwenge wa Uhuru mara baada ya Mwenge huo kuwasili katika eneo la Kalangalala.
Mbunge wa Geita Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akizungumza na wananchi wa Kasamwa mara baada ya miradi ya maendeleo kuzinduliwa katika Halmashauri ya Geita. HABARI na PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA).
---
Mbunge wa Geita Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu,ametoa ahadi ya kuhakikisha kuwa miradi ya maendeleo itakayotekelezwa mwakani katika Halmashauri ya Mji wa Geita itazingatia taratibu zote zinazotakiwa ili isiweze kukataliwa. 

Kauli hiyo imekuja mara baada ya mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu kubaini baadhi ya kasoro katika miradi iliyotekelezwa katika Halmashauri hiyo hali iliyolazimu mradi wa maji kushindwa kuzinduliwa. 

Hayo ameyasema wakati alipokuwa akizungumza na Wananchi wa Kasamwa katika eneo ambalo mkesha wa Mwenge ulipofanyikia katika Halmashauri ya Mji wa Geita mkoani Geita. Kufuatia hali hiyo ya mradi wa maji kushindwa kuzinduliwa unaodaiwa kugharimu shilingi bilioni sita, hali hiyo imempelekea Kiongozi wa mbio za Mwenge wa mwaka huu, Mzee Mkongea Ally kuiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kuchunguza mradi huo . 

Mhe.Kanyasu amesema mwaka huu ukimbizaji Mwenge umekuwa na maana kubwa kufuatia kufanya ukaguzi usiotia shaka kwenye miradi iliyotekelezwa na pale wanapobaini ukiukwaji miradi hiyo imekuwa haizinduliwi. 

"Ukaguzi mnaoufanya katika miradi hii ni ishara tosha kabisa kuwa mmekuja kufanya kazi kwa ajili ya wananchi'' alisisiiza Kanyasu 

Amesema miaka ya nyuma zoezi la ukimbizaji Mwenge lilikuwa la kawaida hali iliyopelekea kila miradi iliyotekelezwa kuzinduliwa bila kujalisha thamani ya pesa inayoendana na miradi halisi. " Mimi binafsi niliweza kupata bahati ya kukimbiza Mwenge wa Uhuru hapo nyuma kidogo, Tulikuwa hatufanyi ukaguzi makini kama unaofanyika mwaka huu. 

Akizungumzia kuhusu kasoro zilizojitokeza katika miradi ya mwaka huu, Mhe.Kanyasu amesema kasoro zote zilizojitokeza mwaka huu hazitajirudia katika Halmashauri hiyo, hivyo ameahidi kuzifanyia kazi. 

Katika hatua nyingine, Mhe, Kanyasu amesema mkoa wa Gieta ni nyumbani kwa Mhe, Rais, Joseph Pombe Magufuli hivyo mwaka ujao atahakikisha hakuna miradi wowote utakaotaliwa kwa vile ni aibu kwao.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: