Happiness Stephen Makala,mkazi wa mtaa wa Busulwa kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga anaomba msaada wa matibabu kwa mtoto wake aitwaye Rogathe Cyprian Makala mwenye umri wa miaka 18, ambaye anayesumbuliwa na tatizo la ugonjwa wa ngozi kwa muda wa miaka 16 sasa.

Anasema amehanghaika katika hospitali mbalimbali hapa nchini, lakini siku moja alikutana na Daktari Bingwa kutoka Apolo India katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga ndipo akampima na kumgundua kuwa homoni zake ziko kwenye njia ya mkojo, hivyo anatakiwa apatiwe matibabu ndani ya miezi tisa kwa kupatiwa dawa kutoka India, ambapo kila mwezi inatakiwa shilingi 504,000 ambapo kwa miezi hiyo tisa ni sawa na shilingi milioni 4.5 (4,536,000/-).

Kwa mujibu wa Daktari huyo,binti  huyo akifikisha umri wa miaka 20 ugonjwa huo wa ngozi utaweza kugeuka na kuwa kansa, na ataweza pia kuwa anazaa watoto wenye kisukari, na kichwa kikubwa na hata kuambukiza watu wengine kwa njia ya kuchangia choo.

Daktari huyo huwa anakuja kila baada ya mwezi hapa mkoani Shinyanga ambapo dozi ya dawa hiyo anatakiwa aanze Juni 2 mwaka huu ambapo itakuja na daktari huyo.

Mama wa binti huyo anasema yeye hana uwezo wa kumtibu binti yake, mume wake alishafariki kwenye ajali mwaka (2007) ambaye alikuwa Mhasibu wa shirika la umeme TANESCO mkoani Shinyanga.

Mama wa mtoto anasema mwanae huwa halali usiku kucha anashinda anajikuna tu na hata wakati wa jua kali huku vipele vikimtoka mwili mzima, na anatarajia kujiunga na kidato cha tano kwani amefaulu kidato cha nne.

Kwa yeyote atakayeguswa kumsaidia awasiliane kwa namba zifuatazo:

Vodacom : 0764206669 ukitaka kutuma kwa m-pesa jina litasoma Happines Makala

Halotel: 0626845953 jina litasoma Eliud Makala
Happines Stephen Makala (kushoto) akiwa na mtoto wake Rogathe Cyprian Makala (18) ambaye anasumbuliwa na ugonjwa wa ngozi na kuomba msaada wa matibabu.
Msichana Rogathe Cyprian Makala akionyesha namna ugonjwa huo wa ngozi unavyomsumbua na kutoka vipele mwili mzima na hawezi kulala usiku akishinda ana jikuna na kuomba msaada wa fedha za matibabu shilingi milioni 4.5
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: