Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na wabunge wakifurahia katika mazungumzo na Peter Mollel maarufu kwa jina la Pierre Konki Liquid (katikati) kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Aprili 3, 2019. Wengine kutoka kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum, Mariamu Ditopile, Mbunge wa Viti Maalum, Munde Tambwe, Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais na Mbunge wa Singida Mjini, Mussa Sima, Mbunge wa Kiembesamaki, Ibrahim Raza na Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa Pierre Liquid ataambatana na Timu ya Taifa, Taifa Stars katika fainali za AFCON zitakazofanyika nchini Misri.
Amemhakikishia hilo wakati akizungumza naye katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma, ambapo Piere alikwenda kutembelea kwa mwaliko wa Spika wa Bunge, Job Ndugai.
Hayo yanajiri ikiwa zimepita siku kadhaa tangu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kutoa kauli ya kukosoa tabia ya watu kuvipa muitikio mkubwa vitu visivyo na msingi, akitolea mfano Mchekeshaji huyo aliyejizolea umaarufu kwenye vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii.
Katika hafla iliyoandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo ambayo ilikuwa na malengo ya kutokomeza ziro katika wilaya hiyo, Makonda alisema kwamba watu wa 'hovyo' kama Pierre hawapaswi kupewa nafasi kwenye vyombo vya habari, hali iliyozua gumzo kubwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments: