Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akiangalia uchimbaji wa mitaro kwa ajili ya ulazaji wa mabomba ya inchi 8 yeye urefu wa Kilomita 2.5 kutoka kwenye tenki la Mabwepande kwa ajili ya kuanza kuwahudumia wananchi wa maeneo ya Bunju, Kitunda na Mabwepande. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akipata maelezo toka kwa wahandishi wanaosimamia mradi wa maji kutoka kwenye tenki la Mabwepande kwa ajili ya kuanza kuwahudumia wananchi wa maeneo ya Bunju, Kitunda na Mabwepande.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja (katikati) akikagua toleo linalopokea maji kutoka Tenki la maji la Mabwepande litakalohudumia wananchi wa Bunju, Kitunda na Mabwepande.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akiongea na wanahabari mara baada ya kumaliza kukagua ulazaji wa mabomba na kukagua toleo linalopokea maji kutoka Tenki la maji la Mabwepande litakalohudumia wananchi wa Bunju, Kitunda na Mabwepande.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja (katikati) akipata maelezo toka kwa Kaimu Meneja wa Miradi ya Maji Mhandisi Ramadhani Mtindasi mara baada ya kufika kukagua Tenki la maji la Mabwepande litakalohudumia wananchi wa Bunju, Kitunda na Mabwepande. Pembeni kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Miradi Mhandisi Lydia Ndibalema.
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Ili kuhakikisha wananchi wanapata Majisafi na Salama Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya majiSafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja ameanza ziara ya wiki moja ya kutembelea miradi 41 ya mamlaka hiyo inayoendeshwa kwa fedha za ndani.
Ziara hiyo iliyoanza leo April 9, 2019 ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani imeangalia tathmini ya miezi sita toka kuanza kwa DAWASA mpya.
Akizungumza kabla ya ziara hiyo, Luhemeja amesema kuna miradi 41 inayotekelezwa kwa fedha za ndani ambapo imetenga asilimia 35 ya mapato yao ya kila mwezi kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali.
“Katika kipindi cha miezi sita tumetumia bilioni 15 kwa ajili ya miradi 41 iliyopo kwenye hatua mbalimbali za utekelezaji na mingine ikiwa ni mipya itakayotatua changamoto ya maji kwenye maeneo yaliyokosa mtandao kwa muda mrefu,”amesema Luhemeja.
Amesema lengo kuu la DAWASA ni kuwekeza kwenye mtandao kwa kutumia fedha za ndani na kila mwezi wamekuwa wanatumia bilion 3 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo Gezaulole, Chalinze Mboga, Kisarawe, Kibamba, Kiwalani Pahse 3 na miradi mingine.
Luhemeja ameeleza kuwa kwa sasa Mkoa wa Dar es Salaam upatikanaji wake wa maji ni asilimia 85 ambapo kwa siku yanazalishwa maji Lita milioni 502 kutoka kwenye mtambo wa Ruvu Juu, Ruvu Chini, Mto Kizinga na Visima vilivyojengwa na jamii au watu binafsi.
Ziara ya Afisa Mtendajj Mkuu itamalizika mwishoni mwa wiki hii na inatarajia kuleta faraja kwa wananchi wa maeneo mbalimbali ikiwemo Mabwepande, Bunju na Kitunda ambapo mradi wao unatarajiwa kukamilika Ijumaa hii na wananchi watapata maji kuanzia Jumamosi.
Toa Maoni Yako:
0 comments: