Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mkoani Morogoro, Janeth Machulya akizungumza na Waandishi wa habari leo kuhusu  uchunguzi wa mfumo ukusanyaji wa mapato kwa njia ya Point of sale (POS) na kubaini baadhi ya Wafanyakazi wa Halmashauri hiyo kutokuwa Waaminifu.
---
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mkoani Morogoro (TAKUKURU),imefanya uchunguzi wa mfumo ukusanyaji wa mapato kwa njia ya Point of sale (POS) na kubaini baadhi ya Wafanyakazi wa Halmashauri hiyo kutokuwa Waaminifu.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mkoani Morogoro, Janeth Machulya,amesema kufuatia kufanyika kwa uchambuzi wa mfumo wa ukusanyaji wa mapato kwa njia ya point of sale (pos) wamebaini baadhi ya Halmashauri mkoani Morogoro kuwa na watumishi wasio waadilifu,ambapo katika kipindi cha robo mwaka 2019 januari hadi machi jumla ya fedha kiasi cha shilingi bilioni 2.5 zimefuatiliwa na shilingi milioni 370.2 zikirejeshwa kutoka halmashauri nne za mkoani Morogoro. 

Amesema Halmashauri zilizorejesha fedha hizo ni pamoja na Kilombero imerejesha milioni 355,950,600/= ikifuatiwa na Kilosa milioni 5,952,00/= huku Mvomero wakirejesha milioni 8,731,850/= na Halmashauri ya wilaya ya Morogoro ikirejesha milioni 5,000,000/=, jumla kwa Halmashauri zote nne zikiwa zimerejesha milioni 370,277,650 na kufanya kiasi cha bilioni 2.5 zilizofuatiliwa kupungua na kubaki bilioni 2.1 ambapo Takukuru Morogoro imeahidi kuzifuatilia na watakaoshindwa kurejesha fedha hizo hatua kali zitachukuliwa dhidi yake. 

Kufuatia zoezi hilo takukuru morogoro imeanza kuchukua hatua kwa kuanzisha uchunguzi ambapo mpaka sasa jumla ya majalada 10 yamefunguliwa. 

“Ningependa kuwakumbusha watumishi wa serikali waliopewa dhamana ya kukusanya mapato na mawakala wote wa Halmashauri za wilaya katika mkoa wa morogoro kuhakikisha kuwa wanawawasilisha benki kwa wakati fedha zote za makusanyo zilizobaki mikononi mwao na maafisa masuhuli kuacha kupanga matumizi ya fedha kabla utaratibu wa kuidhinishwa fedha hizo haujafanywa na mamlaka zinazohusika ” alisema Janeth Machulya. 
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: