Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Mwakilishi wa Umoja wa Afrika kutoka Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, David Phiri wakati alipowasili kufungua Kikao cha Umoja wa Wabunge wa Afrika ya Mashariki wakuangalia Usalama wa Chakula na Lishe tukio lililofanyika leo katika hoteli ya Mount Meru Jijini Arusha. Katikati ni Mwakilishi kutoka Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Ndg. Fred Kafeero
Spika wa Bunge, Job Ndugai akiongozana na Mwakilishi kutoka Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Fred Kafeero (kulia) wakielekea kwenye Ukumbi wa Mkutano kwa ajili ya mazungumzo kabla ya Spika Ndugai kufungua Kikao cha Umoja wa Wabunge wa Afrika ya Mashariki wakuaangalia Usalama wa Chakula na Lishe tukio lililofanyika leo katika hoteli ya Mount Meru Jijini Arusha.
Spika wa Bunge, Job Ndugai (wa pili kulia) akimsikiliza Mwakilishi Umoja wa Afrika kutoka Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, Ndg. David Phiri (kulia) wakati akiwa katika chumba cha mapumziko kabla ya kufungua kikao cha Umoja wa Wabunge wa Afrika ya Mashariki wakuangalia Usalama wa Chakula na Lishe kilichofanyika leo katika hoteli ya Mount Meru Jijini Arusha. Kuanzia kushoto ni Mwakilishi kutoka Umoja wa Afrika Masuala ya Kijamii, Dkt. Margaret Anyetei, Mwenyekiti wa Umoja wa Wabunge wa Afrika ya Mashariki wakuaangalia Usalama wa Chakula na Lishe, Dkt. Abdi Hassan na Mwakilishi kutoka Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Fred Kafeero.
Spika wa Bunge, Job Ndugai akizungumza na Wajumbe Umoja wa Wabunge wa Afrika ya Mashariki wakuangalia Usalama wa Chakula na Lishe wakati wa kikao kilichofanyika leo katika hoteli ya Mount Meru Jijini Arusha.
Wajumbe Umoja wa Wabunge wa Afrika ya Mashariki wakuangalia Usalama wa Chakula na Lishe wakiwa katika kikao kilichofanyika leo katika hoteli ya Mount Meru Jijini Arusha.
Spika wa Bunge, Job Ndugai (katikati) katika picha ya pamoja na Wajumbe Umoja wa Wabunge wa Afrika ya Mashariki wakuangalia Usalama wa Chakula na Lishe tukio lililofanyika leo katika hoteli ya Mount Meru Jijini Arusha. (PICHA NA DEONISIUS SIMBA - OFISI YA BUNGE)
Toa Maoni Yako:
0 comments: