Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Newala Mkoani Mtwara aliposimama kuwasalimia akiwa njiani kuelekea katika chuo cha Ualimu Kitangali kilichopo Wilaya ya Newala Mkoa wa Mtwara ikiwa ni muendelezo wa Ziara yake ya siku tatu Mkoani humo.


Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akiwasalimia Wananchi wa Tandahimba Mkoani Mtwara mara baada ya Msafara wa Rais wa Jamhuri Dkt. John Pombe Magufuli kusimama kwaajili ya kuwasalimia alipokuwa akielekea Kuweka jiwe la msingi la ujenzi katika chuo cha Ualimu cha Kitangali Wilayani Newala Mkoa wa Mtwara. Aprili 3, 2019


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa Canada Nchini Mheshimiwa Pamela O Donnell pamoja na Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako kabla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa chuo cha Kitangali kinachojengwa na Serikali kwa kushirikiana na Canada Wilayani Newala Mkoa wa Mtwara. Aprili 3, 2019
Sehemu ya Majengo ya mapya ya Chuo cha Kitangali ambayo Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa chuo hicho.
Sehemu ya Nyumba za makazi Mapya ya Walimu wa Chuo cha Kitangali ambayo Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa chuo hicho.

PICHA NA IKULU
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: