Hizi ni baadhi ya chaki zinazotengenezwa katika kiwanda Dustless Smart Chalk kilichopo manispaa ya Iringa
Naibu meya wa manispaa ya Iringa Joseph Lyata akiwa kiwandani hapo na kupiga marufuku kwa shule zote za manispaa ya Iringa kununua chaki kutoka nje ya kiwanda Dustless Smart Chalk kilichopo manispaa ya Iringa kwa kuwa kiwanda hicho kinatengeneza chaki zilizo bora.

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

NAIBU meya wa manispaa ya Iringa Joseph Lyata amepiga marufuku kwa shule zote za manispaa ya Iringa kununua chaki kutoka nje ya kiwanda Dustless Smart Chalk kilichopo manispaa ya Iringa kwa kuwa kiwanda hicho kinatengeneza chaki zilizo bora na zinazofaa kutumiwa katika shule zote.

Akizungumza na blog Naibu meya,alisema kuwa kiwanda cha chaki kilichopo katika manispaa ya Iringa kinatengeneza chaki zilizo na kiwango bora cha kutumiwa na walimu wakati wa kufundisha ili kuinua uchumi wa kiwanda hicho.

“Mimi nimekuwa mwalimu kwa takribani miaka nane katika shule mbalimbali na nimefundisha na kuandikia chaki kutoka katika kampuni mbalimbali ila hizi chaki ambazo zinatengemezwa hapa manispaa ya Iringa zinaviwango vinavyotakiwa” alisema Lyata

Lyata alisema kuwa haiwezekani kunakiwanda cha kutengeneza chaki lakini walimu wanatumia chaki kutoka nje ya manispaa ya Iringa kutasababisha kuua mitaji na viwanda hivi vya vijana wabunifu ambao wapo manispaa hapa.

“Tusipo waunga mkono vijana na kiwanda hiki cha kutengeneza chaki tutakuwa tuaua uchumi wa wananchi wa manispaa ya Iringa hivyo lazima walimu wa manispaa ya Iringa kuwaamuru kutumia chaki zinazotengenezwa na kiwanda chetu kilichopo hapa manispaa ya Iringa” alisema Lyata

Aidha Lyata aliwaomba wadau mbalimbali kuendelea kuwasaidia vijana hao wenye kiwanda cha Dustless Smart Chalk ambacho bado kinahitaji vitu vingi ili kuwa na kiwanga kikubwa zaidi na kuongeza ajira kwa vijana wengine.

“Wadau naombe mjaribu kuwatembelea wale vijana walipo pale Ipogolo SIDO kwa kuwa wanafanya kazi kubwa na ubunifu mkubwa kwa lengo la kufanikiwa kuja kuwa na kiwanda kikubwa ambacho kitasaidia kuongeza ajira kwa vijana wengine” alisema Lyata

Lyata alisema kuwa kiwanda cha Dustless Smart Chalk kinakabiliwa na upungufu wa vifaa na vitendea kazi ambavyo vinarudisha nyuma kazi zao hivyo wadau wanatakiwa kujitokeza na kuwasiadia kununua vifaa pamoja kukiboresha kiwanda hicho kuwa cha kimataifa.

Lakini Lyata alimalizia kwa kusema kuwa chaki hizo zinaubora wa kimataifa kwa kuwa hazina vumbi wala madhara kwa binadamu yeyeto yule hivyo sasa ni muda muafaka kwa walimu kutumia chaki hizo.

Awali akitoa taarifa kwa Naibu meya mmoja wa wanakikundi wa kiwanda cha Dustless Smart Chalk Prisca Masalanga alisema kuwa kiwanda hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali hasa za vifaa bora vya kuzalishia bidhaa hii ya chaki.

“Tunazalisha chaki zenye kiwango bora lakini tunakumbana na uhaba wa vifaa vinavyopelekea kuanika chaki hizi kwenye meza kwa kuwa hatuna sehemu sahihi ya kuanikia chaki hizi,bado hatuna mashine kubwa bado tunatumia mashine ndogo” alisema Masalanga

Masalanga alisema kuwa changamoto kubwa ambayo wanakumbana nao ni kukosa soko la kudumu la chaki kutoka katika kiwanda hicho cha Dustless Smart Chalk ambacho kinauwezo wa kuazalisha chaki zenye ubora unaotakiwa kufundishia mashuleni.

“Kwa kweli ndugu mwandishi kiwanda chetu bado hatuna soko tunazalisha tu hizi chaki huku tukitafuta soko na kuwaomba wadau kutusaidia kutafuta soko ili tuweze kuuza chaki hizi na kukuza mitaji yetu na kuwa na kiwanda kikubwa ambacho kitaajili vijana wanzetu wengi hapo baadae” alisema Masalanga
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: